102- Ambaye anamweka kwenye mwanandani wake atasema:

بسم الله، وعلى سنة رسول الله

“Kwa jina la Allaah na kutokana na mwenendo wa Mtume wa Allaah.”

بسم الله، وعلى ملة رسول الله صلى الله عليه وسلم

“Kwa jina la Allaah na kutokana na mila ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Dalili ya hilo ni kwamba Hadiyth ya Ibn ´Umar isemayo:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapomweka maiti ndani ya kaburi basi husema: [Katika tamko lingine imekuja: “Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Mkatapoweka maiti zenu ndani ya makaburi yenu basi semeni:]

بسم الله، وعلى سنة

“Kwa jina la Allaah na kutokana na mwenendo wa Mtume.”

[Katika upokezi mwingine imekuja:

بسم الله، وعلى ملة

“Kwa jina la Allaah na kutokana na mila… ”]

 رسول الله

“… ya Mtume wa Allaah.”

Ameipokea Abu Daawuud (02/70), at-Tirmidhiy (02/152-153), Ibn Maajah (01/470), Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake (773), al-Haakim (01/366), al-Bayhaqiy (04/55), Ahmad (4990, 5233, 537, 6111) kupitia njia mbili kutoka kwa Ibn ´Umar.

Tamko la kwanza ni la Abu Daawuud, Ibn Maajah na Ibn-us-Sunniy. Tamko lingine ni la waliobakia.

Kuhusu upokezi mwingine ni wa at-Tirmidhiy, Ibn Maajah, al-Haakim na upokezi wa Ahmad. Maana ya mapokezi yote mawili ni moja. at-Tirmidhiy amesema:

“Hadiyth ni nzuri.”

al-Haakim amesema na adh-Dhahabiy akaafikiana naye:

“Swahiyh kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim.”

Mambo ni kama walivosema. Upokezi wa baadhi yao juu ya upokezi huo kwamba ni wenye kutoka kwa Swahabah haidhuru kitu kutokana na mambo mawili:

1- Yule ambaye amesema imetoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mwaminifu. Isitoshe ni ziada kutoka kwake. Kwa hivyo ni lazima kuikubali. Aidha inatiliwa nguvu na:

2- Jambo la pili: Imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupitia njia nyingine. Au aseme:

بسم الله، وبالله، وعلى ملة رسول الله صلى الله عليه وسلم

“Kwa jina la Allaah na kwa ajili ya Allaah na kutokana na mila ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Hilo ni kutokana na Hadiyth ya al-Bayaadhwiy (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Maiti anapolazwa ndani ya kaburi lake basi waseme wale wanaomuweka pale wanapomweka katika mwanandani:

بسم الله، وبالله، وعلى ملة رسول الله صلى الله عليه وسلم

“Kwa jina la Allaah na kwa ajili ya Allaah na kutokana na mila ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Ameipokea al-Haakim hali ya kuwa ni yenye kutolea ushahidi Hadiyth ya kabla yake. Cheni ya wapokezi wake ni nzuri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 192-193
  • Imechapishwa: 14/03/2022