Uongozi wa Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) ni miaka miwili na miezi mitatu na nyusiku tisa; kuanzia tarehe 13 Rabiy´ al-Awwal mwaka wa 11 mpaka tarehe 22 Jumaadaa al-Aakhirah mwaka wa 13 baada ya kuhajiri.

Uongozi wa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) ni miaka kumi na miezi sita na siku tatu; kuanzia tarehe 23 Jumaadaa al-Aakhirah mwaka wa 13 mpaka tarehe 26 Dhul-Hijjah mwaka wa 23 baada ya kuhajiri.

Uongozi wa ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) ni miaka kumi na mbili isipokuwa siku kumi na mbili; kuanzia tarehe 01 Muharram mwaka wa 24 mpaka tarehe 18 Dhul-Hijjah mwaka wa 35 baada ya kuhajiri..

Uongozi wa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) ni miaka minne na miezi tisa; kuanzia tarehe 19 Dhul-Hijjah mwaka wa 35 mpaka tarehe 19 Ramadhaan mwaka wa 40 baada ya kuhajiri..

Jumla ya uongozi wa wote hawa ni miaka ishirini na tisa, miezi sita na siku nne.

al-Hasan bin ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa) alipewa kiapo cha usikivu siku aliyokufa baba yake (Radhiya Allaahu ´anh) katika Rabiy´ al-Awwal mwaka wa 41 baada ya kuhajiri. Alimwachia uongozi Mu´aawiyah. Hivyo ikadhihiri miujiza ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale aliposema:

“Uongozi baada yangu utakuwa kwa miaka thelathini.”[1]

“Hakika mwanangu huyu ni bwana. Hakika Allaah atasuluhisha kupitia kwake makundi mawili makubwa ya waislamu.”[2]

Ameipokea al-Bukhaariy.

al-Hasan ni mjukuu wake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na rehani lake. Yeye ni kiongozi wa waumini mtoto wa kiongozi wa waumini ambaye ni ´Aliy bin Abiy Twaalib. Alizaliwa tarehe 15 Ramadhaan mwaka wa 03 na akafa al-Madiynah na akazikwa al-Baqiy´ katika Rabiy´ al-Awwal mwaka wa 50 baada ya kuhajiri.

al-Husayn ni mjukuu wake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na rehani lake. Naye ni mwana wa ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh). Alizaliwa Shawwaal mwaka wa 04 na akauliwa Karbalaa tarehe 10 Muharram mwaka wa 61 baada ya kuhajiri.

Thaabit ambaye ni Qays bin Shammaas al-Answaariy al-Kharraaj ambaye alikuwa ni muhubiri wa Answaar. Aliuliwa hali ya kuwa shahidi siku ya al-Yamaamah mwaka wa 11 baada ya kuhajiri mwishoni mwake au mwanzoni mwa mwaka wa 12 baada ya kuhajiri.

[1] Abu Daawuud (4646), at-Tirmidhiy (2226), Ahmad (5/221), at-Twabaraaniy katika “al-Kabiyr” (6444), al-Hakiym (3/145) na wengineo.

[2] al-Bukhaariy (2704).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 143-144
  • Imechapishwa: 14/12/2022