Nimepata dalili nyingi ndani ya Qur-aan na Sunnah zinazotilia nguvu yale ninayosema. Kuhusu Qur-aan Allaah (Ta´ala) anasema kuhusu watu wa Kitabu:

وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ فَنَبَذُوهُ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ وَاشْتَرَوْا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَبِئْسَ مَا يَشْتَرُونَ

“Wakati alipochukua Allaah fungamano la wale waliopewa Kitabu [akawaambia:] “Bila shaka mtakibainisha kwa watu na wala hamtokificha. Lakini walikitupa nyuma ya migongo yao na wakakibadilisha kwa thamani ndogo. Basi ubaya ulioje kwa yale wanayoyanunua.”[1]

26 – al-Ashja´iy ametuhadithia, kutoka kwa Maalik bin Mighwal, kutoka kwa ash-Sha´biy ambaye amesema kuhusu Aayah hii:

“Ilibaki mikononi mwao lakini hata hivyo wakaacha kuifanyia kazi.”

Baada ya hapo Allaah akatuhalalishia kula vichinjwa vyao na kuwaoa wanawake zao. Akawahukumu kuwa hukumu ya Kitabu kwa sababu walikuwa wenye kukikubali na akawanasibishia nacho. Wanaingizwa ndani ya Kitabu kwa upande wa hukumu na jina, licha ya kwamba wanatofautiana nacho inapokuja katika uhakika wenyewe. Hii ni dalili iliyopo ndani ya Qur-aan.

[1] 3:187

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 81-82
  • Imechapishwa: 04/07/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naawswir-ud-Diyn al-Albaaniy