Kwetu sisi jambo zima linatakiwa kufahamika kwa njia ya kwamba maasi na madhambi hayaiondoshi imani na wala hayapelekei katika ukafiri; yanachofanya ni kuondosha ule uhakika na utakasifu wa imani ambao Allaah amewasifia wenye nayo na akawashurutishia nayo katika maeneo mengi ndani ya Kitabu Chake ikiwa ni pamoja na:

إِنَّ اللَّـهَ اشْتَرَىٰ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ ۚ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ

”Hakika Allaah amenunua kwa waumini nafsi zao na mali zao kwamba watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Allaah; wanaua na wanauawa.”[1]

Baada ya hapo akasema (Ta´ala):

التَّائِبُونَ الْعَابِدُونَ الْحَامِدُونَ السَّائِحُونَ الرَّاكِعُونَ السَّاجِدُونَ الْآمِرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَالنَّاهُونَ عَنِ الْمُنكَرِ وَالْحَافِظُونَ لِحُدُودِ اللَّـهِ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ

”Wanaotubia, wanaofanya ‘ibaadah, wanaomuhimidi, wanaofunga, wanaorukuu, wanaosujudu, wanaoamrisha mema na wanaokataza maovu na wanaohifadhi mipaka ya Allaah; na wabashirie waumini.”[2]

قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ وَالَّذِينَ هُمْ عَنِ اللَّغْوِ مُعْرِضُونَ وَالَّذِينَ هُمْ لِلزَّكَاةِ فَاعِلُونَ وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ وَالَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَوَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْوَارِثُونَ الَّذِينَ يَرِثُونَ الْفِرْدَوْسَ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ

”Hakika wamefaulu waumini; ambao katika swalah zao wananyenyekea, na ambao wanajiepusha na mambo ya upuuzi, na ambao wanatoa zakaah, na ambao wanazihifadhi tupu zao; isipokuwa kwa wake zao, au kwa iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi. Lakini atakayetaka kinyume ya hayo, basi hao ndio wachupao mipaka. Na ambao amana zao na ahadi zao wanazichunga, na ambao wanazihifadhi swalah zao – hao ndio warithi, ambao watarithi al-Firdaws, wao humo ni wenye kudumu.”[3]

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقًّا

“Hakika si venginevyo waumini ni wale ambao anapotajwa Allaah, basi nyoyo zao zinajaa khofu na wanaposomewa Aayah Zake huwazidishia imani na kwa Mola wao wanategemea; ambao wanasimamisha swalah na hutoa sehemu katika yale tuliyowaruzuku. Hao ndio Waumini wa kweli!  Wana ngazi [za juu] kwa Mola wao na msamaha na riziki tukufu.”[4]

Aayah zimebainisha na kuweka wazi mambo ya Shari´ah Yake aliyowafaradhishia watu wake na akaikanushia maasi yote. Kisha Sunnah ikazifasiri kwa Hadiyth ambazo zinataja sifa za imani na ambazo nimezitaja mwanzoni mwa kitabu hiki. Wakati maasi yanapochanganyika na imani hii iliyoelezwa, hukosa zile sharti na sifa ambazo Allaah amewafaradhishia nazo waumini na zile alama wanazotambulika kwazo. Kwa hivyo ikaondoka ile hakika yake licha ya kwamba jina bado linatumika kwao.

Huenda mtu akauliza inawezekanaje kusema kuwa mtu sio muumini ingawa bado yuko na imani, jibu ataambiwa kuwa jambo hilo linaendana kabisa na lugha ya kiarabu ambalo tumelihifadhi kwa njia nyingi. Hakuna yeyote anayepinga kuwa matendo ya mtendaji yanakanushwa yanapofanywa pasi po uhakika wake. Huoni namna husema kumwambia mtengenezaji asipofanya kazi nzuri kwamba hakufanya chochote? Kwa msemo mwingine hakufanya kazi nzuri, na si kwamba hakufanya kazi kabisakabisa. Wanamzingatia kuwa amefanya kazi kwa upande wa jina, lakini hakufanya kazi yoyote kwa upande wa umairi. Kwa ajili hiyo wanaweza kumsema kwa zaidi ya haya. Hilo ni kama mfano wa mtu ambaye anamuasi mzazi wake na kumfanyia maudhi ambapo akamkana kuwa si mwanae, ilihali kila mtu anajua kuwa ni mtoto wake kabisa. Hayo pia yanaweza kusemwa juu ya ndugu, mke na mtumwa. Malengo ni kuonyesha kuwa hawakubaliani na ule utiifu waliyowajibishiwa.

Kuhusu ndoa, utumwa na nasaba, yanabaki kama yalivyokuwa katika maeneo na majina yake. Vivyo hivyo kuhusu madhambi haya ambayo yanapelekea imani kukanushwa, kwa sababu mambo ya Shari´ah ndio imekanusha uhakika wake ambayo ni katika sifa zake. Majina yanabaki kama yalivyokuwa hapo kabla – hawaitwi jengine zaidi ya waumini na hivyo ndivo watahukumiwa.

[1] 9:111

[2] 9:112

[3] 23:1-11

[4] 8:2-4

  • Mhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 78-81
  • Imechapishwa: 04/07/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naawswir-ud-Diyn al-Albaaniy