06 – Kueneza siri

Mwanamke anaweza kuwa mwenye kubwabwaja. Mdomoni mwake hakubaki kitu katika yale yaliyotokea kati yake yeye na mume wake. Ni mamoja maneno hayo ni muhimu au sio muhimu. Kwa hiyo anawasambazia marafiki zake matukio mbalimbali yanayoendelea baina yake yeye na mume wake. Mdomoni mwake hakubaki kitu. Pengine anamweleza siri hizo rafiki yake au mama yake. Lakini wakati mwingine mwanaume ndiye anayepewa mtihani huo. Pengine yeye ndiye mwenye kubwabwaja. Mfano wa hali kama hizi waume hawawapendi wake kama hawa ambao hawabakizi siri za nyumbani. Akimfanyia subira mwezi au mwaka huenda asisubiri maisha yake yote na akalazimika kutoa talaka ili kuepuka shari yake.

  • Mhusika: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Twalaaq – asbaabuhu wa ´ilaajuh, uk. 25-26
  • Imechapishwa: 03/04/2024