Amesmea:

 وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا أَيْنَ شُرَكَاؤُكُمُ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ثُمَّ لَمْ تَكُن فِتْنَتُهُمْ إِلَّا أَن قَالُوا وَاللَّـهِ رَبِّنَا مَا كُنَّا مُشْرِكِينَ

”Siku Tutakayowakusanya wote pamoja kisha tutawaambia wale walioshirikisha: “Wako wapi washirika wenu ambao mlikuwa mkidai?” Hapo haitokuwa fitina yao isipokuwa kusema: “Tunaapa kwa Allaah, ee Mola wetu, hatukuwa washirikina!”[1]

Watakanusha ya kwamba walikuwa washirikina. Amesema katika Aayah nyingine:

يَوْمَئِذٍ يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَعَصَوُا الرَّسُولَ لَوْ تُسَوَّىٰ بِهِمُ الْأَرْضُ وَلَا يَكْتُمُونَ اللَّـهَ حَدِيثًا

“Siku hiyo wale waliokufuru na wakamuasi Mtume watatamani lau ardhi isawazishwe juu yao;  na wala hawatoweza kumficha Allaah chochote katika yale waliyosema [au kufanya].”[2]

Hivyo wakaitilia mashaka Qur-aan na wakadai kuwa ni yenye kujigonga.

Kuhusu maneno Yake:

وَاللَّـهِ رَبِّنَا مَا كُنَّا مُشْرِكِينَ

“Tunaapa kwa Allaah, ee Mola wetu, hatukuwa washirikina!”

pindi wataona jinsi Allaah anavyowasamehe wapwekeshaji, basi washirikina wataambiana:

”Akituuliza, basi tuseme kuwa hatukuwa washirikina.”[3]

Wakati Allaah atawakusanya pamoja na masanamu yao atasema:

أَيْنَ شُرَكَاؤُكُمُ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ

“Wako wapi washirika wenu ambao mlikuwa mkidai?”

Atasema:

ثُمَّ لَمْ تَكُن فِتْنَتُهُمْ إِلَّا أَن قَالُوا وَاللَّـهِ رَبِّنَا مَا كُنَّا مُشْرِكِينَ

”Hapo haitokuwa fitina yao isipokuwa kusema: “Tunaapa kwa Allaah, ee Mola wetu, hatukuwa washirikina!”

Wataponyamaza, ataipiga muhuri midomo yao na badala yake kuamrisha viungo vyao vya mwili kuzungumza. Hiyo ndio maana ya maneno Yake:

الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَىٰ أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُم بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ

”Leo Tunatia vizibo juu ya vinywa vyao, na mikono yao itusemeshe na miguu yao itoe ushahidi kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.”[4]

Allaah (´Azza wa Jall) akakhabarisha viungo vyao vitavyoshuhudia. Hiyo ndio tafsiri ya yale ambayo wameyatilia mashaka mazanadiki[5].

[1] 6:22-23

[2] 4:42

[3] Mujaahid amesema:

“Yatasemwa na washirikina watapoona jinsi madhambi yanasamehewa, lakini Allaah hatowasamehe washirikina.” (Tazama “ad-Durr al-Manthuur” (3/259) ya as-Suyuutwiy)

[4] 36:65

[5] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 71-73
  • Imechapishwa: 03/04/2024