Amesema katika Aayah moja:

وَإِنَّ يَوْمًا عِندَ رَبِّكَ كَأَلْفِ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونَ

”… na hakika siku moja kwa Mola wako ni kama miaka elfu katika ile mnayoihesabu.”[1]

Katika Aayah nyingine amesema:

يُدَبِّرُ الْأَمْرَ مِنَ السَّمَاءِ إِلَى الْأَرْضِ ثُمَّ يَعْرُجُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ أَلْفَ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونَ

”Anayaendesha mambo kutoka mbinguni mpaka ardhini, kisha inapanda Kwake katika siku ambayo kipimo chake ni sawa na miaka elfu katika yale mnayoihesabu nyinyi.”[2]

Akasema tena katika Aayah nyingine:

تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ

”Malaika na Roho wanapanda Kwake katika siku kipimo chake ni sawa na miaka elfu khamsini.”[3]

Wanauliza ni vipi maneno haya yatakuwa ya wazi ilihali yanagongana?

Ama kuhusu Aayah:

وَإِنَّ يَوْمًا عِندَ رَبِّكَ كَأَلْفِ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونَ

”… na hakika siku moja kwa Mola wako ni kama miaka elfu katika ile mnayoihesabu.”[4]

inahusiana na zile siku ambazo Allaah ameziumba mbingu na ardhi; kila siku moja ni sawa na miaka elfu.

Aayah nyingine inasema:

يُدَبِّرُ الْأَمْرَ مِنَ السَّمَاءِ إِلَى الْأَرْضِ ثُمَّ يَعْرُجُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ أَلْفَ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونَ

”Anayaendesha mambo kutoka mbinguni mpaka ardhini, kisha inapanda Kwake katika siku ambayo kipimo chake ni sawa na miaka elfu katika yale mnayoihesabu nyinyi.”

Jabraaiyl alikuwa akiteremka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kisha akipanda tena katika siku ambayo ni sawa na miaka mia tano, kwa sababu masafa kati ya mbingu na ardhi kuna mwendo wa miaka mia tano; kushuka miaka mia tano na kupanda miaka mia tano na jumla inakuwa miaka elfu.

Aayah isemayo:

تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ

”Malaika na Roho wanapanda Kwake katika siku kipimo chake ni sawa na miaka elfu khamsini.”

Bi maana endapo angelikuweko mwingine asiyekuwa Allaah ambaye anawafanyia hesabu viumbe, basi asingelimaliza isipokuwa baada ya miaka elfu khamsini. Ndio maana Allaah atawafanyia hesabu viumbe wote kwa kiasi cha nusu ya siku katika siku za dunia. Hiyo ndio maana ya maneno Yake (Ta´ala):

وَكَفَىٰ بِنَا حَاسِبِينَ

”Inatosheleza Kwetu kuwa wenye kuhesabu.”[5]

Bi maana kasi ya kufanya hesabu[6].

[1] 22:47

[2] 32:5

[3] 70:4

[4] 22:47

[5] 21:47

[6] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 69-71
  • Imechapishwa: 03/04/2024