Amesema:

رَبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ

”Mola wa mashariki na wa magharibi.”[1]

رَبُّ الْمَشْرِقَيْنِ وَرَبُّ الْمَغْرِبَيْنِ

”Mola wa mashariki mbili na Mola wa magharibi mbili.”[2]

فَلَا أُقْسِمُ بِرَبِّ الْمَشَارِقِ وَالْمَغَارِبِ

”Basi naapa kwa Mola wa mashariki na magharibi!”[3]

Wakaitilia shaka Qur-aan na kuhoji ni vipi inakuwa hivo katika maneno ya wazi.

Kuhusu Aayah isemayo:

َبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ

”Mola wa mashariki na magharibi.”

inahusiana na ile siku ambayo usiku utalingana na mchana, ambapo Allaah akaapa kwa mashariki na magharibi Yake.

Aayah:

رَبُّ الْمَشْرِقَيْنِ وَرَبُّ الْمَغْرِبَيْنِ

”Mola wa mashariki mbili na Mola wa magharibi mbili.”

inakusudia siku ndefu zaidi na fupi zaidi katika mwaka, ambapo Allaah akaapa kwa mashariki zake mbili na magharibi zake mbili.

Aayah:

فَلَا أُقْسِمُ بِرَبِّ الْمَشَارِقِ وَالْمَغَارِبِ

”Basi naapa kwa Mola wa mashariki na magharibi!”[4]

inahusiana na mashariki ya mwaka na magharibi ya mwaka. Haya ndio waliyoyatilia mashaka mazanadiki[5].

[1] 26:28

[2] 55:17

[3] 70:40

[4] 70:40

[5] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 68-69
  • Imechapishwa: 03/04/2024