108. Rawaatib zinazoswaliwa kwa mnasaba wa swalah za faradhi

Rawaatib zinazoswaliwa kwa mnasaba wa swalah za faradhi ni Rak´ah kumi na moja:

1 – Rak´ah nne kabla ya Dhuhr.

2 – Rak´ah mbili baada yake.

3 – Rak´ah mbili baada ya Maghrib.

4 – Rak´ah mbili baada ya ´Ishaa.

5 – Rak´ah mbili kabla ya Fajr.

Umm Habiybah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia kuwa amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Hakuna mja muislamu anayeswali kwa ajili ya Allaah kila siku Rak´ah kumi na mbili kwa kujitolea pasi na zile za faradhi, isipokuwa Allaah atamjengea nyumba Peponi.”

Imekuja katika tamko jengine:

“Yeyote anayeswali Rak´ah kumi na mbili mchana na usiku basi Allaah atamjengea kwazo nyumba Peponi.”

Ameipokea Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 229
  • Imechapishwa: 03/04/2024