10. Ni ipi hukumu ya mchezo wa karata na sataranji?

Swali 10: Ni ipi hukumu ya mchezo wa karata na sataranji?

Jibu: Wanazuoni (Rahimahumu Allaah) wamesema kuwa michezo hiyo ni haramu, kama walivoyataja hayo wanazuoni wetu. Hilo ni kutokana na ule upotofu mwingi unaopatikana katika jambo hilo na kuzuia kutokamana na utajo wa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Pengine vilevile likapelekea katika uadui na chuki kati ya wachezaji. Mara nyingi michezo hii inachezwa kwa zawadi, inatambulika ya kwamba kucheza kwa ajili ya zawadi ni jambo halijuzu isipokuwa katika yale mambo yaliyotajwa na Shari´ah, nayo ni mambo matatu: kulenga shabaha, khofu na kwato. Yule mwenye kuzingatia hali za wachezaji sataranji na karata, basi ataona kuwa wanapoteza wakati mrefu katika mambo yasiyokuwa ya kumtii Allaah na yasiyokuwa na faida. Baadhi ya watu wanasema kuwa kucheza karata na sataranji unafungua ubongo na kuikuza akili, lakini ukweli mambo ni kinyume na vile wanavyodai watu hawa. Bali ni jambo linadumaza akili na kuifanya akili ni yenye kufupika. Ikiwa mtu atazitumia fikira zake kwa njia nyingine, hatopata kitu, kwa sababu akili imedumazwa na kufupika katika jambo hili. Kwa ajili hiyo ni lazima kwa mwenye busara kujiepusha na michezo hiyo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah Muhimmah, uk. 18
  • Imechapishwa: 01/03/2023