Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Lakini waliwafanya baadhi ya viumbe kuwa wakati na kati baina ya wao na Allaah (Ta´ala). Wanasema kuwa wanataka kutoka kwao wawakurubishe mbele ya Allaah (Ta´ala) na kwamba wanataka uombezi wao Kwake [Allaah]; kama mfano wa Malaika, ´Iysaa, Maryam na wengineo katika watu wema.
MAELEZO
Wao walikuwa wakiyaabudu masanamu haya ili wajikurubishe tu mbele ya Allaah. Walikuwa wakikubali wenyewe kuwa waungu hawa wako chini ya Allaah, na kwamba hawamiliki kuwanufaisha wala kuwadhuru na kwamba wao ni waombezi wao tu mbele ya Allaah (´Azza wa Jall). Lakini uombezi huu ni batili na haumfai kitu mwenye nao. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ
“Basi hautowafaa uombezi wowote ule wa waombezi.” (74:48)
Allaah (Ta´ala) haridhii shirki ya washirikina hawa. Ni jambo lisilowezekana Akawaachia wawaombee. Hakuna uombezi isipokuwa kwa yule ambaye Allaah (´Azza wa Jall) atamridhia. Allaah haridhii kwa mja Wake ukafiri na wala hapendi ufisadi. Kwa hivyo kitendo cha washirikina kufungamana na waungu wao ambao wanawaabudu ni batili na hayana maana yoyote. Wanasema:
هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ
“Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.” (10:18)
Kitendo hichi hakizidishi kwa Allaah jengine isipokuwa kuwa mbali zaidi na Allaah. Haya ni kutokamana na ujinga na upumbavu wao wanajaribu kujikurubisha mbele ya Allaah kwa nyombezi batili ambazo haziwazidishii jengine isipokuwa kuwaweka mbali kabisa na Allaah.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Utaymiyn
- Mfasiri: Fitqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 21
- Imechapishwa: 23/04/2022

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Utaymiyn
Mfasiri: Fitqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 21
Imechapishwa: 23/04/2022
https://firqatunnajia.com/10-mlango-01-washirikina-wa-kiarabu-wanaabudu-waombezi-pamoja-na-allaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)