10. Kutofoautiana kwa watu inapokuja katika shahaadah

Mwenye kutamka neno hili na huku akawa anajua maana yake, akitendea kazi muqtadha yake kukiwemo kupinga shirki na kumthibitishia Allaah umoja pamoja vilevile na kuyaamini hayo na kuyatendea kazi, basi huyo ndiye muislamu wa kweli.

Mwenye kulitamka na akatendea kazi muqtadha yake kwa uinje pasi na kuliamini ndani ya moyo wake, basi huyo ni mnafiki.

Mwenye kulitamka kwa ulimi wake na akatendea kazi shirki ambayo ndio kinyume chake na ambayo pia inapingana na yale yanayofahamishwa nalo, huyo ni kafiri. Haijalishi kitu ijapokuwa atalisema mara kwa mara na kwa kukariri. Hivo ndivyo ilivyo hali ya waabudu makaburi ambao wanalitamka neno hili na hawafahamu maana yake. Neno hili halina athari yoyote kwao katika kutengeneza mwenendo wao na kurekebisha matendo yao. Utawaona wanasema “hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah” na wakati huohuo wanasema:

“Niokoe, ee ´Abdul-Qaadir!”, “Niokoe, ee al-Badawiy”, “Niokoe, ee fulani na fulani!” Wanawakimbilia wafu na wanawaomba uokozi wakati wa majanga.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 17
  • Imechapishwa: 25/03/2019