Ibn Taymiyyah akifafanua kilichozuka (حديث) katika Qur-aan

Akitumia hoja kwa maneno Yake:

مَا يَأْتِيهِم مِّن ذِكْرٍ مِّن رَّبِّهِم مُّحْدَثٍ

“Hakuna ukumbusho wowote ule mpya unaowajia kutoka kwa Mola wao… “[1]

Ataambiwa kuwa Aayah hii ni hoja dhidi yake. Kwani pindi anaposema (Ta´ala):

مَا يَأْتِيهِم مِّن ذِكْرٍ مِّن رَّبِّهِم مُّحْدَثٍ

“Hakuna ukumbusho wowote ule mpya unaowajia kutoka kwa Mola wao… “[2]

ikapata kufahamika kuwa kuna ukumbusho kutoka Kwake ambao unakuwa mpya na ukumbusho mwingine ambao sio mpya. Kwa sababu maelezo yanapotajwa kwa njia isiyokuwa ya hakika mtu anapata kujua kuwa yanatofautiana na maelezo mengine. Ni kama mfano wa kusema:

“Hatonijia mtu ambaye ni muislamu isipokuwa nitamtukuza.”

Hivyo imepata kufahamika kuwa kilichozuka katika Aayah hakikuumbwa kama wanavodai Jahmiyyah. Hata hivyo inahusiana na kipya kilichoteremka. Kwani Allaah alikuwa akiteremsha Qur-aan hatua baada ya hatua…

Katika suala hili la kimsingi Ahl-us-Sunnah wanatofautiana na Jahmiyyah katika Mu´tazilah, wanafalsafa na wengineo.

[1] 21:02

[2] 21:02

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/279-280)
  • Imechapishwa: 25/03/2019