10. Kila mmoja katika Ahl-us-Sunnah anayaamini haya

34- Shaykh-ul-Islaam Abul-Hasan ´Aliy bin Ahmad bin Yuusuf al-Qurashiy al-Hakaariy ametaja: Abul-Qaasim ´Abdullaah bin al-Hasan bin Muhammad bin al-Khallaal ametuhadithia: Muhammad bin al-´Abbaas al-Mukhlisw ametuhadithia: Abu Bakr bin Abiy Daawuud ametuhadithia: ar-Rabiy´ bin Sulaymaan ametuhadithia:

“Niilimuuza ash-Shaafi´iy (Radhiya Allaahu ´anh) kuhusu sifa miongoni mwa sifa za Allaah (Ta´ala) ambapo akajibu: “Ni haramu kwa akili kumlinganisha Allaah (Ta´ala), akili kumfanyia kikomo, dhana kumkatia, nafsi kumfikiria, dhamiri kuingia kwa undani, mawazo kumzunguka na ubongo kumwelewa vyengine isipokuwa vile Alivyojisifu Mwenyewe katika Kitabu Chake au kupitia kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

35- Yuunus bin ´Abdil-A´laa amesema:

“Nilimsikia Abu ´Abdillaah Muhammad bin Idriys ash-Shaafi´iy (Radhiya Allaahu ´anh) akisema wakati alipoulizwa kuhusu sifa na yale anayoamini ambapo akasema: “Allaah (Ta´ala) ana majina na sifa zilizotajwa katika Kitabu Chake na ambazo Mtume Wake  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewaeleza Ummah wake. Si haki kwa yeyote katika viumbe wa Allaah ambaye amefikiwa na hoja kuyarudisha. Kwa sababu yamekuja na Qur-aan na yamesihi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupitia wapokezi waaminifu. Mwenye kukhalifu hayo baada ya kuthibitikiwa na hoja ni kafiri. Ama kabla ya kuthibitikiwa na hoja ni mwenye kupewa udhuru kwa sababu ya ujinga wake kwa sababu ni mambo yasiyoweza kutambulika kwa kutumia akili, kuonekana wala fikira. Hatumkufurishi yeyote ambaye ni mjinga kabla ya kufikiwa na hoja.”

36- Ibn Wadhdhwaah amesema:

“Kila mmoja ambaye nimekutana naye katika Ahl-us-Sunnah anasadikisha Hadiyth kuhusu kushuka. Ibn Ma´iyn amesema:

“Isadikishe na wala usiieleze.”

Amesema vilevile:

“Ikubali bila kuifanyia kikomo.”

37- Imepokelewa kwamba al-Hasan al-Baswriy amesema:

“Mutwarrif amezungumza maneno ambayo yalisemwa kabla yake na hayatosemwa baada yake. Wakasema: “Amesema nini, ee Abu Sa´iyd?” Akasema: “Amesema: “Shukurani zote za dhati zimwendee Allaah ambaye katika kumuamini ni kutoyajua yale ambayo hakujisifu Mwenyewe.”

38- Sahnuun amesema:

“Katika kumjua Allaah ni kunyamazia yale ambayo hakujisifu Mwenyewe.”

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dhamm-ut-Ta’wiyl, uk. 20-22
  • Imechapishwa: 13/12/2018