Miongoni mwa mambo yanayotilia nguvu kutofautiana kwa imani kutokana na matendo, ni maneno Yake Allaah (´Azza wa Jall):

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقًّا

“Hakika si venginevyo waumini ni wale ambao anapotajwa Allaah, basi nyoyo zao zinajaa khofu na wanaposomewa Aayah Zake huwazidishia imani na kwa Mola wao wanategemea; ambao wanasimamisha swalah na hutoa sehemu katika yale tuliyowaruzuku. Hao ndio Waumini wa kweli!  Wana ngazi [za juu] kwa Mola wao na msamaha na riziki tukufu.”[1]

Allaah hakufanya uhakika wa imani isipokuwa kwa matendo kutokana na sharti hizi. Ambaye anadai kuwa inatosha mtu kuwa muumini wa kweli hata kama hakufanya matendo, basi anaifanyia inda Qur-aan na Sunnah. Miongoni mwa mambo yanayofahamisha kutofautiana kwa imani ndani ya moyo, ni maneno Yake Allaah (´Azza wa Jall):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا جَاءَكُمُ الْمُؤْمِنَاتُ مُهَاجِرَاتٍ فَامْتَحِنُوهُنَّ

”Enyi mlioamini! Wanapokujieni waumini wa kike waliohajiri, basi wajaribuni.”[2]

Huoni kuwa hapa kuna ngazi inayofautiana na ngazi nyingine:

اللَّـهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِهِنَّ ۖ فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ ۖ لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ

“Allaah anajua zaidi imani zao. Mkiwatambua kuwa ni waumini wa kike, basi msiwarejeshe [Makkah] kwa makafiri – wao si [wake] halali kwao [hao makafiri] na wala wao si [waume] halali kwao.”[3]?

Vivyo hivyo mfano wa maneno Yake Allaah (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا آمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَالْكِتَابِ الَّذِي نَزَّلَ عَلَىٰ رَسُولِهِ وَالْكِتَابِ الَّذِي أَنزَلَ مِن قَبْلُ ۚ وَمَن يَكْفُرْ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا

“Enyi mlioamini! Mwaminini Allaah na Mtume Wake na Kitabu alichokiteremsha kwa Mtume Wake na Kitabu alichokiteremsha kabla. Na atakayemkufuru Allaah na Malaika Wake na Vitabu Vyake na Mitume Yake na siku ya Mwisho, basi kwa hakika amepotoka upotofu wa mbali.”[4]

Kungelikuwa hakuna nafasi ya kuzidi, basi kusingelikuwa na maana yoyote ya kuamrisha imani. Allaah (Subhaanah) amesema tena:

أَحَسِبَ النَّاسُ أَن يُتْرَكُوا أَن يَقُولُوا آمَنَّا وَهُمْ لَا يُفْتَنُونَ وَلَقَدْ فَتَنَّا الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۖ فَلَيَعْلَمَنَّ اللَّـهُ الَّذِينَ صَدَقُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْكَاذِبِينَ

“Je, wanadhani watu kwamba wataachwa [bila kupewa mitihani] kwa kuwa wanasema: “Tumeamini.” basi ndio wasijaribiwe?” Kwa hakika Tuliwajaribu wale wa kabla yao ili Allaah awatambulishe wale waliosadikisha na ili awatambulishe waliokadhibisha.”[5]

Vilevile amesema (Ta´ala):

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ فَإِذَا أُوذِيَ فِي اللَّـهِ جَعَلَ فِتْنَةَ النَّاسِ كَعَذَابِ اللَّـهِ

”Miongoni mwa watu wako wasemao “Tumemwamini Allaah”; lakini wanapofanyiwa maudhi kwa ajili ya Allaah, hufanya mitihani ya watu kama kwamba ni adhabu ya Allaah.”[6]

Amesema (Tabaarak wa Ta´ala) tena:

وَلِيُمَحِّصَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَيَمْحَقَ الْكَافِرِينَ

“… na ili Allaah awajaribu walioamini na awafutilie mbali makafiri.”[7]

Huoni namna ambavyo (Tabaarak wa Ta´ala) anawapa watu mtihani kwa kusadikisha maneno kwa kitendo? Amesema (´Azza wa Jall) hakuridhia kule kutambua kwao pasi na matendo – Ameyafanya ni kitu kimoja. Ni kitu gani mtu anatakiwa kufuata baada ya Qur-aan, Sunnah na mfumo wa Salaf ambao ndio nafasi ya kuigilizwa na uongozi?

´Aqiydah ambayo sisi tunashikamana nayo ni ile iliyothibitishwa na kuandikwa katika kitabu chetu hichi, ya kwamba imani ni kwa nia, maneno na matendo vyote kwa pamoja na kwamba ni ngazi mbalimbali. Licha ya kwamba ya kwanza na ngazi ya juu kabisa ni kushuhudia kwa kutamka ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, kama alivosema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth ambayo amefanya imani ni tanzu sabini na kitu. Kwa hivyo pindi mtamkaji atakapotamka shahaadah na akakubali ujumbe uliotoka kwa Allaah, basi anakuwa muumini kwa njia ya kupambana na kukamilika kwake na si kwa njia ya kujisifu. Kila ambavyo atazidi kumtii na kumcha Allaah, ndivo itakavyozidi imani yake.

[1] 8:2-4

[2] 60:10

[3] 60:10

[4] 4:136

[5] 29:2-3

[6] 29:10

[7] 3:141

  • Mhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 32-35
  • Imechapishwa: 21/06/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naawswir-ud-Diyn al-Albaaniy