09 – Yahyaa bin Sa´iyd ametuhadithia, kutoka kwa Abul-Ashhab, kutoka kwa al-Hasan ambaye amesema:

“Kuna bwana mmoja alimwambia Ibn Mas´uud: “Mimi ni muumini.” Ibn Mas´uud akamuuliza: “Je, wewe ni katika watu wa Peponi?” Bwana yule akasema: “Nataraji.” Ndipo Ibn Mas´uud akasema: “Kwa nini basi hujasema hivo tangu mwanzo?”[1]

10 – ´Abdur-Rahmaan bin Mahdiy ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan bin Sa´iyd, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Abu Waa-il ambaye amesema:

“Bwana mmoja alikuja kwa ´Abdullaah akasema: “Wakati tulipokuwa tunatembea tulikutana na wapanda farasi ambapo tukawauliza: “Ni kina nani nyinyi?” Akasema: “Sisi ni waumini.” Ndipo akasema: “Walitakiwa kusema kuwa ni katika watu wa Peponi.”[2]

11 – Yahyaa bin Sa´iyd och Muhammad bin Ja´far ametuhadithia, kutoka kwaa Shu´bah, kutoka kwa Salamah bin Kuhayl, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Alqamah ambaye amesema:

“Bwana mmoja alisema kumwambia ´Abdullaah: “Mimi ni muumini.” Ndipo ´Abdullaah akasema: “Sema pia kwamba uko Peponi. Sivyo hivyo, lakini tunamwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake na Mitume Yake.”

12 – ´Abdur-Rahmaan ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Muhill bin Mihraz[3] ambaye amesema:

“Ibraahiym alinambia: “Mtu akikuuliza kama wewe ni muumini, basi mjibu kwa kusema: “Namwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake na Mitume Yake.”

13 – ´Abdur-Rahmaan ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Ma´mar, kutoka kwa Ibn Twaawuus, kutoka kwa baba yake aliyesema:

“Mtu akikuuliza kama wewe ni muumini, basi jibu kwa kusema: “Namwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake na Mitume Yake.”

 14 – ´Abdur-Rahmaan ametuhadithia, kutoka kwa Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Yahyaa bin ´Atiyq, kutoka kwa Muhammad bin Siyriyn ambaye amesema:

“Mtu akikuuliza kama wewe ni muumini, basi jibu kwa kusema:

آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَمَا أُوتِيَ النَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُون

“Tumemwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl na Ishaaq na Ya’quub na al-Asbaatw na aliyopewa Muusa na ‘Iysaa na waliyopewa Manabii kutoka kwa Mola wao, hatutofautishi baina ya mmoja yeyote miongoni mwao nasi Kwake tunajisalimisha.”[4]

15 – Jariyr bin ´Abdil-Hamiyd ametuhadithia, kutoka kwa Mansuur, kutoka kwa Ibraahiym ambaye amesema:

“Mtu mmoja alimuuliza ´Alqamah kama ni muumini. Akajibu: “Nataraji hivo – Allaah akitaka.”

[1] Wapokezi wake ni waaminifu, lakini cheni ya wapokezi imekatika kati ya al-Hasan na Ibn Mas´uud. Abul-Ashhab alikuwa anaitwa Ja´far bin Hayyaan.

[2] Cheni ya wapokezi wake ni kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim. Vivyo hivyo kuhusu cheni ya wapokezi inayofuata. Upokezi huu upo katika ”Kitaab-ul-Iymaan” (122) cha Ibn Abiy Shaybah kupitia njia nyingine kutoka kwa Abu Waaiyl.

[3] Alikuwa anatokea Kuufah na hana neno.

[4] 2:136

  • Mhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 35-38
  • Imechapishwa: 21/06/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naawswir-ud-Diyn al-Albaaniy