10. Hadiyth “Yule mwenye kuniswalia mara moja, basi Allaah atamwandikia mema kumi… “

10 – ´Aliy bin ´Abdillaah ametuhadithia: Yaziyd bin al-Habbaab ametuhadithia: Muusa bin ´Ubaydah amenihadithia: Qays bin ´Abdir-Rahmaan bin Abiy Swa´swa´h amenihadithia, kutoka kwa Sa´d bin Ibraahiym, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf, aliyesema:

كان لا يفارق فيء النبي صلى الله عليه وسلم بالليل والنهار خمسة نفر من أصحابه أو أربعة لما ينوبه من حوائجه، قال: فجئت فوجدته قد خرج فتبعته، فدخل حائطاً من حيطان الأسواف فصلى فسجد سجدة أطال فيها فحزنت وبكيت فقلت: لأرى رسول الله صلى الله عليه وسلم قد قبض الله روحه، قال: فرفع رأسه، وتراءيت له، فدعاني، فقال: ما لك؟ قلت: يا رسول الله سجدت سجدة أطلت فيها فحزنت، وبكيت، وقلت: لأرى رسول الله صلى الله عليه وسلم قد قبض الله روحه قال: (هذه سجدة سجدتها شكراً لربي فيما آتاني في أمتي، من صلى عليَّ صلاة كتب الله له عشر حسنات).

”Walikuwepo Maswahabah wanne au watano wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao walikuwa hawatengani naye usiku na mchana kwa ajili ya kumtimizia haja zake. Siku moja nikamwendea nikamkuta ametoka ambapo nikamfuata. Akaingia kwenye bustani ya Aswaaf[1] ambapo akaswali na kusujudu sijda refu. Nikahuzunika, nikalia na kusema: ”Nadhani kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Allaah ameichukua roho yake.” Ndipo akanyanyua kichwa chake. Nikajionyesha kwake ambapo akaniita. Akasema: ”Una nini?” Nikasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Hakika umesujudu sijda refu. Nikahuzunika, nikalia na kusema: ”Nadhani kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Allaah ameichukua roho yake.” Ndipo akasema: ”Hii ni sujuud ambayo nimesujudu kwa ajili ya kumshukuru Mola wangu kwa ya yale aliyonipa juu ya ummah wangu. Yule mwenye kuniswalia mara moja, basi Allaah atamwandikia mema kumi.”[2]

[1] Ibn-ul-Athiyr amesema:

”Ni jina la maeneo patukufu pa Madiynah ambapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipafanya patukufu.” (an-Nihaayah)

Katika ”al-Lisaan” imekuja:

”Imesemekana vilevile kuwa ni mahali pembezoni mwa al-Baqiy´.”

[2] Hadiyth ni Swahiyh kupitia njia zake na zingine zinazoitia nguvu. Moja katika njia hizo (07) imekwishatangulia huko mwanzo.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 28-29
  • Imechapishwa: 15/03/2023