09. Hadiyth ”Yule mwenye kuniswalia mara moja… “

9 – ´Iysaa bin Miynaa’ ametuhadithia: Muhammad bin Ja´far ametuhadithia, kutoka kwa al-´Alaa’, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

من صلَّى عليَّ صلى الله عليه عشراً

”Yule mwenye kuniswalia mara moja, basi Allaah atamswalia mara kumi.”[1]

[1] Swahiyh. Hata hivyo kuna maneno machache juu ya Miynaa.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 28
  • Imechapishwa: 15/03/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy