289 – ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

أمر رسول الله صلى الله عليه وسلم رجلا يصلى بالناس الظهر فتفل في القبلة، وهو يصلى للناس، فلما كانت صلاة العصر أرسل إلى آخر، فأشفق الرجل الأول، فجاء إلى النبى صلى الله عليه وسلم فقال: يا رسول الله: أأُنزل في شيءٌ؟ قال: لا، ولكنك تفلت بين يديك وأنت قائمٌ تؤُّمُّ الناس، فآذيت الله والملائكة

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha bwana mmoja awaswalishe watu Dhuhr. Akatema mate Qiblah na huku anawaswalisha watu. Wakati ilipofika ´Aswr, akamteua mtu mwingine. Yule mtu wa kwanza akaogopa ambapo akaenda kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema: “Ee Mtume wa Allaah! Kumeteremshwa juu yangu chochote?” Akasema: “Hapana, lakini wewe ulitema mate mbele yako ilihali unawaswalisha watu. Hivyo ukawa umemuudhi Allaah na Malaika.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” kwa cheni ya wapokezi nzuri.

[1] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/236)
  • Imechapishwa: 16/11/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy