09. Hadiyth “Bwana mmoja aliwaswalisha watu akatema mate kwenye Qiblah… “

288 – Mmoja katika Maswahabah zake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa jina Abu Sahlah as-Saaib bin Khallaad amesimulia:

أن رجلاً أمَّ قوماً فبصق في القبلة، ورسول الله صلى الله عليه وسلم ينظر، فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم حين فرغ: لا يصلى لكم هذا ، فأراد بعد ذلك أن يُصلى لهم فمنعوه وأخبروه بقول رسول الله صلى الله عليه وسلم، فذكر ذلك لرسول الله صلى الله عليه وسلم؟ فقال: نعم، وحسبتُ أنه قال: إنك آذيت الله ورسوله

“Bwana mmoja aliwaswalisha watu akatema mate kwenye Qiblah ambapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamuona. Alipomaliza kuswali Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Asikuswalisheni huyu.” Baada ya tukio hilo akataka kuwaswalisha, wakamzuia na wakamweleza alivosema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Baadaye Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaambiwa jambo hilo ambapo akasema: “Ndio.” Nadhania pia alisema kwamba: “Hakika wewe umemuudhi Allaah na Mtume Wake.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake.

[1] Swahiyh kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/235)
  • Imechapishwa: 16/11/2022
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy