Picha katika zama kabla ya kuja Uislamu zilikuwa nyingi na zinazotukuzwa badala ya Allaah. Hali iliendelea hivo mpaka pale Allaah alimtumiliza Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akayavunja masanamu, akazifuta picha na Allaah akamfanya kuitokomeza shirki na njia zake. Kila anayetengeneza picha, akaisimamisha au akaitukuza basi amejifanaisha na makafiri katika yale waliyoyafanya na amewafungulia watu mlango wa shirki na njia zake. Yule atakayeamrisha picha na akaridhika nazo, basi hukumu yake ni kama ya yule mtendaji katika kukemewa na kustahiki matishio. Kwa sababu ni jambo limethibiti ndani ya Qur-aan, Sunnah na maneno ya wanazuoni kuharamishwa kuamrisha maasi na kuridhika nayo kama ilivyoharamishwa kuyatenda. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَىٰ مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ

”Unapowaona wale wanaoziingilia na kuzishambulia Aayah Zetu, basi jitenge nao mpaka waingie kwenye mazungumzo mengineyo. Na kama shaytwaan akikusahaulisha, basi baada ya kukumbuka usikae pamoja na watu madhalimu.”[1]

وَقَدْ نَزَّلَ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ أَنْ إِذَا سَمِعْتُمْ آيَاتِ اللَّـهِ يُكْفَرُ بِهَا وَيُسْتَهْزَأُ بِهَا فَلَا تَقْعُدُوا مَعَهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ إِنَّكُمْ إِذًا مِّثْلُهُمْ

”Naye amekwishakuteremshieni katika Kitabu kwamba mnaposikia Aayah za Allaah zinakanushwa na zinafanyiwa istihzai, basi msikae pamoja nao mpaka waingie katika mazungumzo mengineyo. Vinginevyo mtakuwa kama wao.”[2]

Aayah imejulisha kuwa yule mwenye kuhudhuria maeneo kunapofanywa maovu na asiwapinge wenye nayo, basi hukumu yake ni moja kama wao.

Ikiwa yule ambaye ananyamazia maovu – licha ya kuweza kuyakemea au kuwatenga – anakuwa ni kama wale watendaji, basi jambo la kuamrisha maovu au kuyanyamazia dhambi yake inakuwa kubwa zaidi kuliko mnyamazaji, mwenye hali mbaya zaidi na mwenye haki zaidi ya kuwa mfano wa wale watendaji. Dalili zenye maana kama hii ni nyingi anazipata yule anayezitafuta maeneo pake.

Kutokana na zile Hadiyth na maneno ya wanazuoni tuliyoyataja katika jawabu hili inapata kumbainikia ambaye anakusudia haki ya kwamba kule kukunjuka kwa watu katika kuchukua picha viumbe vilivyo na roho katika vitabu, magazeti, majarida na vijitabu ni kosa la wazi na ni maasi ya wazi. Ni lazima kwa yule anayeitakia mema nafsi yake kutahadhari na jambo hilo na kuwatahadharisha ndugu zake kutokamana na jambo hilo. Ayafanye hayo baada ya kutubu tawbah ya kweli kutokana na yaliyotangulia. Vilevile inamdhihirikia kutokana na zile dalili zilizotangulia kuwa haijuzu zikabaki picha hizi zinazoashiriwa katika hali yake. Bali ni lazima kukata au kufuta kichwa chake muda wa kuwa haziko katika zulia na kitu mfano wake katika vile vitu vinavyokanyagwa na kutwezwa. Katika hali hiyo itafaa kuiacha katika hali yake kama dalili ya hilo ilivyotangulia katika Hadiyth zilizopokelewa na ´Aaishah na Abu Hurayrah.

[1] 06:68

[2] 04:140

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Jawaab al-Mufiyd fiy Hukm-it-Taswwiyr kutoka katika Majmuu´-ul-Fataawaa (04/219-221)
  • Imechapishwa: 28/03/2022