09. Vitu vyenye kupita vinavyokata swalah

09- Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Vifuatavyo vinakata swalah ya mtu endapo havitokuwa mbele yake kama kiti cha nyuma cha tandiko la ngamia; mwanamke (anayepata hedhi[1]), punda na mbwa mweusi.” Abu Dharr amesema: “Ee Mtume wa Allaah! Ni ipi tofauti kati ya mbwa mweusi na mbwa mwekundu?” Akasema: “Mbwa mweusi ni shaytwaan.”[2]

[1] Bi maana mwanamke aliyebaleghe. Vinakata swalah ina maana kwamba inabatilika. Hadiyth inayosema “Hakuna kinachokata swalah.” ni dhaifu, kama nilivyochambua katika “Tamaam-ul-Minnah”, uk. 306, na kwenye vitabu vingine.

[2] Muslim, Abuu Daawuud na Ibn Khuzaymah (2/95/1). Tazama vitabu vyangu ”Tahdhiyr-us-Saajid min Ittikhaadh-il-Qubuur al-Masaajid” na ”Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´auha”.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 74
  • Imechapishwa: 13/10/2016