Hakika kipimo kilichokusudiwa, lau ingelikubaliwa usahihi wake yenyewe, basi sharti la kukikubali na kukijengea hoja ni pale ambapo kinakuwa hakipingani na Sunnah. Ama ikiwa kinapingana nayo, kama ulivyoona mwenyewe, basi haijuzu kukiangalia. Kwa sababu hiyo imesemwa kwamba yanapokuja masimulizi, basi hubatilika mtazamo, na unapokuja mto wa Allaah basi hubatilika mto wa Ma´qal. Mtu asemeje ilihali kipimo hicho kinapingana na maneno ya khaliyfah mwongofu ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh)? Uzoefu wangu kwa wale wanaofuata kichwa mchunga ni kwamba huacha kushikamana na Sunnah Swahiyh inapopingana na maneo yake (Radhiya Allaahu ´anh), kama walivyofanya katika talaka tatu kwa mpigo, basi vipi wayachukue maneno yake pale yalipoafikiana na Sunnah? Abu ´Uthmaan an-Nahdiy amesema:
”Nilikutana na Sa´d na Ibn ´Umar wakibishana kwa ´Umar kuhusu kufuta juu ya soksi za ngozi. ´Umar akasema: ”Afute juu yake mpaka mfano wa wakati wake uleule wa mchana na usiku wake.”[1]
Hapa kuna dalili ya wazi juu ya kwamba kufuta huanza tangu pale anapopangusa soksi kwa mara ya kwanza mpaka wakati mfano wake uleule wa mchana na usiku. Kwa kadiri ninavyojua, masimulizi yote kutoka kwa Maswahabah, ambayo ameyapokea ´Abdur-Razzaaq katika ”al-Muswannaf”, yanaonekana namna hii. Kwa mfano amepokea kwamba ´Amr bin al-Haarith amesema:
”Nilisafiri pamoja na ´Abdullaah kwenda al-Madaain. Akapangusa juu ya soksi za ngozi siku tatu bila kuzivua.”[2]
Kutokana na yale niliyoyasema masimulizi ya Salaf yameenda sambamba na Sunnah zake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – basi shikamana nayo utakuwa – kwa idhini ya Allaah – umeongoka.
[1] ´Abdur-Razzaaq (1/209/807). Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa masharti ya al-Bukhaariy na Muslim.
[2] ´Abdur-Razzaaq (1/180). Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa masharti ya al-Bukhaariy na Muslim.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Itmaam-un-Nush fiy Ahkaam-il-Mash, uk. 91-92
- Imechapishwa: 27/04/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Itmaam-un-Nush fiy Ahkaam-il-Mash, uk. 91-92
Imechapishwa: 27/04/2026
https://firqatunnajia.com/09-sunnah-inapokuja-yanabatilika-maoni-yote/