70- Hasan bin Qaasim al-Azraqiy amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisimama juu ya mpando wa mlima wa Tabuuk na kusema: “Hapa ndio Shaam” akaashiria Shaam na “Hapa ndio Yemen” akaashiria al-Madiynah.”[1]

71- al-Waaqidiy amesema katika “al-Maghaaziy” bila ya mlolongo wa wapokezi ya kwamba bonde la Quraa ndio mpaka kati ya Shaam na Hijaaz na vingine vyote kwenda chini mpaka al-Madiynah ni Hijaaz.

72- Ibn Hibbaan amesema katika “as-Swahiyh” yake:

“Shaam inapanuka kutoka Baalis mpaka al-´Ariysh Misri.”

73- Mu´aadh bin Jabal amesema:

“Ardhi takasifu inapanuk kuanzia Jerusalemu mpaka Aufrat.”

Lakini hata hivyo mlolongo wa wapokezi wake si Swahiyh.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameiombea du´aa Shaam na kusema:

“Ee Allaah! Tubarikie Shaam yetu! Ee Allaah! Tubarikie Yemen yetu!” Wakasema: “Na Najd yetu.” Akasema: “Ee Allaah! Tubarikie Shaam yetu! Ee Allaah! Tubarikie Yemen yetu!” Wakasema: “Na Najd yetu.” Ndipo akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Huko kuna tetemeko na mitihani na huko kutatokea pembe la shaytwaan.”[2]

[1] al-Haakim (4/555) na at-Twabaraaniy (7717). Ibn Kathiyr amesema: “Tafsiri ya kwamba Shaam inapanuka kuanzia Tabuuk ni bora kuliko tafsiri ya al-Waliyd inayosema kuwa inapanuka kuanzia Yerusalemu na Allaah ndiye anajua zaidi.” (Tafsiyr-ul-Qur-aan al-´Adhwiym (03/54))

[2] al-Bukhaariy (990).

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Baghdaadiy al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-ush-Shaam, uk. 87-89
  • Imechapishwa: 10/02/2017