Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَأَوْرَثْنَا الْقَوْمَ الَّذِينَ كَانُوا يُسْتَضْعَفُونَ مَشَارِقَ الْأَرْضِ وَمَغَارِبَهَا الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا

“Tukawarithisha watu waliokuwa wakikandamizwa mashariki mwa ardhi na magharibi mwake ambayo Tumeibariki.”[1]

Allaah amewarithisha wana wa israaiyl Shaam.

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَىٰ بِعَبْدِهِ لَيْلًا مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ

“Utakasifu ni wa ambaye amemsafirisha usiku mja Wake kutoka al-Masjid al-Haraam kwenda mahala pa kuswalia mbali ambao Tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake.”[2]

وَجَعَلْنَا بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ الْقُرَى الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا قُرًى ظَاهِرَةً وَقَدَّرْنَا فِيهَا السَّيْرَ ۖ سِيرُوا فِيهَا لَيَالِيَ وَأَيَّامًا آمِنِينَ

”Baina yao na miji tuliyoibariki, Tuliweka miji mingine iliyodhihirika na tukakadiria humo vituo vya safari [Tukawaambia:] ”Safirini humo usiku na mchana kwa amani.”[3]

54- ´Ubayy bin Ka´b amesema kuhusiana na maneno ya Allaah:

وَنَجَّيْنَاهُ وَلُوطًا إِلَى الْأَرْضِ الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا لِلْعَالَمِينَ

“Tukamuokoa na Luutw kuelekea ardhi ambayo tumeibariki kwa ajili ya walimwengu.”[4]

“Bi maana Shaam. Hakuna maji yoyote matamu isipokuwa yanatiririka kutoka katika mwamba ule Yerusalemu.”

55- al-Hasan al-Baswriy amesema kuhusiana na maneno ya Allaah:

وَأَوْرَثْنَا الْقَوْمَ الَّذِينَ كَانُوا يُسْتَضْعَفُونَ مَشَارِقَ الْأَرْضِ وَمَغَارِبَهَا الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا

“Tukawarithisha watu waliokuwa wakikandamizwa mashariki mwa ardhi na magharibi mwake ambayo Tumeibariki.”[5]

“Bi maana mashariki ya Shaam na magharibi yake.”

Vivyo hivyo ndivyo amesema Zayd bin Aslam, Qataadah na Sufyaan.

56- as-Suddiy amesema kuhusiana na maneno ya Allaah:

وَلِسُلَيْمَانَ الرِّيحَ عَاصِفَةً تَجْرِي بِأَمْرِهِ إِلَى الْأَرْضِ الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا ۚ وَكُنَّا بِكُلِّ شَيْءٍ عَالِمِينَ

“Na kwa Sulaymaan Tulimfanyia upepo wa kimbunga unaokwenda kwa amri yake katika ardhi tulioibarikia; Nasi tulikuwa kwa kila jambo ni Wenye kukijua.”[6]

“Bi maana Shaam.”

57- Ka´b-ul-Ahbaar amesema:

“Allaah ameibariki Shaam kutoka Eufrat mpaka al-´Ariysh.”

58- Kuna mwanamme mmoja alikuja kwa Ka´b-ul-Ahbaar na kumwambia kuwa anataka kutoka kusafiri kwa ajili ya kutafuta fadhila za Allaah. Ndipo akasema:

“Nenda Shaam! Baraka haipungui kokote duniani isipokuwa inaongezeka Shaam.”

59- ´Abdul-Malik al-Jazariy amesema:

“Ikiwa dunia imekumbwa na majanga na ukame basi Shaam kunakuwa na raha na kuzuri. Ikiwa Shaam imekumbwa na majanga na ukame basi Yerusalemu kunakuwa na raha na kuzuri. Shaam imebarikiwa, Palestina ni takatifu na Jerusalemu takasifu ya takasifu.”

60- Thawr bin Yaziyd amesema:

“Ardhi takasifu zaidi ulimwenguni ni Shaam, ardhi takasifu zaidi ya Shaam ni Palestina, ardhi takasifu zaidi ya Palestina ni Yerusalemu, ardhi takasifu zaidi Yerusalemu ni juu ya mlima, ardhi takasifu zaidi ya mlima ni msikiti na ardhi takasifu zaidi ya msikiti ni kuba.”

61- Tambua ya kwamba baraka Shaam inajumuisha ya kidini na ya kidunia. Kwa ajili hii ndio maana ikaitwa ardhi Takatifu. Allaah (Ta´ala) alisema ya kwamba Muusa (´alayhis-Salaam) amesema:

يَا قَوْمِ ادْخُلُوا الْأَرْضَ الْمُقَدَّسَةَ الَّتِي كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ

“Enyi watu wangu, ingieni ardhi iliyotakaswa ambayo Allaah amekuhukumieni!”[7]

62- Imaam Ahmad amepokea kupitia kwa Abu Dharr aliyesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Utafanya nini ukifukuzwa kutoka al-Madiynah?” Nikasema: “Basi nitaishi kwa raha na amani na kwenda zangu na kuwa njiwa katika njiwa za Makkah.” Ndipo akasema: “Utafanya nini ukifukuzwa kutoka Makkah?” Nikasema: “Basi nitaishi kwa raha na amani na kwenda zangu Shaam na ardhi Takatifu.” Akasema: “Utafanya nini ukifukuzwa kutoka Shaam?” Nikasema: “Ninaapa kwa Yule aliyekutuma kwa haki ya kwamba nitauweka upanga wangu juu ya bega langu.” Akasema: “Au kilicho bora kuliko hicho? Sikiliza na utii hata kama atakuwa mja wa kihabeshi.”

63- Abud-Dardaa’ alimwandikia Salmaan:

“Njoo katika ardhi Takatifu! Ardhi ya Jihaad!”

64- Qataadah amesema:

“Ardhi takatifu ni Shaam.”

65- ´Ikrimah na as-Suudiy wamesema:

“Ardhi takatifu ni Ariyhaa.”

66- al-Kalbiy amesema:

“Ardhi takatifu ni Dameski na Palestina.”

67- Makusudio ya takasifu ni kwamba imesafika kutokamana na shirki na yale yanayoipelekea. Kwa ajili hiyo ndio maana ikawa ni ardhi ya Mitume.”

68- Dhwamrah bin Rabi´ah amesema:

“Nimesikia ya kwamba hakuna Mtume yeyote isipokuwa anatokea Shaam. Akiwa si mwenye kutokea huko huka huko kupitia safari ya usiku.”

69- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Qur-aan imeteremshwa sehemu tatu; Makkah, al-Madiynah na Shaam.”

al-Waliyd amesema:

“Bi maana Yerusalemu.”

Ameipokea al-Haakim ambaye amesema kuwa mlolongo wa wapokezi wake ni Swahiyh.

Allaah ameiita Shaam mazuri na ya salama pindi Aliposema:

وَلَقَدْ بَوَّأْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ مُبَوَّأَ صِدْقٍ

“Hakika wana wa israaiyl Tuliwapa makazi mazuri na salama.”[8]

Qataadah amesema:

“Aliwafanya kuishi Shaam na Yerusalemu.”

[1] 07:137

[2] 17:01

[3] 34:18

[4] 21:71

[5] 07:137

[6] 21:81

[7] 05:21

[8] 10:93

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Baghdaadiy al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-ush-Shaam, uk. 83-87
  • Imechapishwa: 10/02/2017