Maelezo yote ya Salaf kuhusu masuala kama haya ni jambo lenye manufaa sana. Hii ni kwa sababu mkusanyiko wa maelezo yao yote unaonyesha vyema zaidi makusudio kuliko maelezo moja au mawili. Hata hivyo lazima kuwepo na tofauti za msingi miongoni mwao, kama vile zinavyopatikana tofauti katika hukumu mbalimbali za Kishari´ah. Tunajua kwamba masuala mengi ambayo wengi miongoni mwa watu wamekhitilafiana yanatambulika vyema kwa wote – bali yamepokelewa kwa mapokezi mengi kwa watu wa kawaida na wanazuoni. Hii ni kama idadi ya Rak´ah za swalah, kiwango chake na nyakati zake, ufaradhi wa zakaah na viwango vyake, kuilengesha Ramadhaan, Twawaaf, kusimama ´Arafah, kurusha vijiwe kwenye Nguzo, vituo na kadhalika. Tofauti za maoni miongoni mwa Maswahabah, kama kuhusu masuala ya urithi kati ya babu na ndugu wa aliyekufa, urithi wa ndugu, kushirikiana katika urithi na mfano wake hazisababishi shaka yoyote katika masuala ya msingi ya mirathi. Allaah ameteremsha Aayah tatu zinazofafanua masuala ya mirathi ambazo watu wengi wanahitaji, ikiwa ni pamoja na mirathi ya wazazi, mirathi ya watoto, mirathi ya ndugu wasio na watoto na mirathi ya wanandoa. Katika ya kwanza Amewataja wazazi na vizazi vyao, katika ya pili Ametaja warithi wanaorithi urithi uliowekwa na ya tatu Ametaja warithi wasiorithi urithi uliowekwa, nao ni wale ndugu wa baba na mama tumbo moja au wale wa baba pekee. Ni mara chache babu na ndugu wote kuwa hai wakati mwosia anapokufa. Kwa ajili hiyo jambo hilo halikutokea katika Uislamu isipokuwa baada ya kufariki kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Tofauti za maoni zinaweza kujitokeza kwa sababu ya udhaifu wa dalili. Zinaweza kujitokeza kwa sababu watu hawakuzisikia. Sababu nyingine ni kuifahamu kimakosa. Kwa kuongeza inaweza kutokana na kuamini kwamba kuna hoja yenye nguvu inayopingana. Madhumuni hapa ni kufafanua maelezo ya jumla ya jambo hili pasi na kuingia kwenye maelezo ya kina.
- Muhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr, uk. 46-47
- Imechapishwa: 31/03/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
“Kuna tofauti katika masuala haya” – mbinu chafu ya al-Ikhwaan al-Muslimuun
Swali: Watu walioathirika na fikira za al-Ikhwaan al-Muslimuun daima wanajengea hoja kwa mfumo wa kukusanya/kulegeza (التمييع) kwa njia ya tofauti na kwamba wanazuoni wametofautiana ili zisikaripiwe zile Bid´ah na makosa walionayo. Unasemaje juu ya hilo? Jibu: Kuna tofauti kati ya tofauti za wanazuoni za hapo kale na tofauti za sasa.…
In "al-Waadi´iy kuhusu maandamano, uasi, mapinduzi na migomo"
10. Mahimizo ya umoja ndani ya matendo ya Salaf
Kuhusu matendo ya Salaf hakika miongoni mwa misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jmaa´ah juu ya masuala yenye tofauti muda wa kuwa tofauti hizo zinatokana na Ijtihaad na isitoshe ikawa inafaa kufanya Ijtihaad katika mambo hayo, basi baadhi wanawapa udhuru wengine kwa tofauti hizo. Hilo halipelekei baadhi kuwajengea wengine chuki, uadui wala bughudha.…
In "Sharh Usuwl-is-Sittah - Ibn ´Uthaymiyn"
15. Hadiyth Swahiyh isiyokuwa na shaka yoyote
Kwa hiyo ikiwa Hadiyth imesimuliwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kutoka vyanzo viwili tofauti, pamoja na kutambua ya kwamba mmoja wao hakuichukua kutoka kwa mwingine, basi inathibitishwa kuwa ni Swahiyh, khaswa ikiwa inatambilika kwamba wapokezi wake si watu wanaojulikana kusema uwongo makusudi na kubwa liliopo ni kwamba…
In "Muqaddimah fiy Usuwl-it-Tafsiyr"