Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Suala la tatu: Kuilingania.

MAELEZO

Bi maana kulingania katika elimu na matendo. Mbora wa watu ni yule aliyejua, akafanyia kazi na akawalingania wengine juu ya elimu na matendo. Amesema (´Azza wa Jall):

وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِّمَّن دَعَا إِلَى اللَّهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِينَ

“Na nani mwenye kauli nzuri zaidi kuliko yule anayelingania watu kwa Allaah na akatenda mema na akasema: “Hakika mimi ni miongoni mwa waislamu?”[1]

Kulingania kwa Allaah, kutendea kazi kwa Shari´ah ya Allaah na kunyenyekea na kujisalimisha na amri ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala).

[1] 41:33

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Twariyqal-Usuwl ilaa idhwaah-ith-Thalaat-il-Usuwl, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 22/11/2021