Hadiyth hii inafahamisha kuwa hakuna nafasi ya kutumia hesabu katika kuthibitisha kuanza na kumalizika kwa mwezi. Shaykh-ul-Islam Ibn Taymiyyah na wengine wameeleza maafikiano ya Maswahabah juu ya hilo[1], kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefungamanisha hukumu na uonaji na si kwa hesabu. Isitoshe kuona kunaweza kufikiwa na kila mtu, mjinga na mjuzi, jambo ambalo ni rehema ya Allaah kwa waja wake na wepesi wake juu yao.

[1] Tazama ”al-Fataawaa” (25/207) na “Fath-ul-Baariy” (4/127).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/13)
  • Imechapishwa: 30/01/2025