Ama yale yaliyomo ndani ya vitabu vya Fiqh kwamba hapana vibaya kutengeneza picha ikiwa ni katika kitu kinachotandikwa chini, wamejengea hoja juu ya kwa Hadiyth ya ´Aaishah na Hadiyth ya Abu Hurayrah:
”Tukafanya baadaye mto mmoja au mito miwili.”
na:
”Amrisha pazia ikatwe na kufanywe mito miwili inayokanyagwa chini.”
Katika hayo kuna dalili ya kujuzu kubaki kwa picha zilizotengenezwa ikiwa zimefanywa kuwa vitu vya chini kama tandiko au mto. Lakini hilo halifahamishi kuwa inajuzu kutengeneza picha katika vitu hivyo. Bali kutengeneza picha ni haramu kwa mtengenezaji wake katika hali yoyote ile. Akifanya hivyo, basi amefanya lililoharamishwa. Yule ambaye picha imefika kwake kisha akaifanya kuwa kitu cha kutandikwa chini, basi kwa kufanya hivyo ameondokewa na wajibu wa kukemea ovu juu yake.
Kiasi hiki kinatosha kwa mwenye uongofu – na Allaah ndiye Mwenye kutoa tawfiyq.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin ´Aliy ash-Shawkaaniy (afk. 1250)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Hukm-ut-Taswwiyr, uk. 35-38
- Imechapishwa: 07/05/2026
Ama yale yaliyomo ndani ya vitabu vya Fiqh kwamba hapana vibaya kutengeneza picha ikiwa ni katika kitu kinachotandikwa chini, wamejengea hoja juu ya kwa Hadiyth ya ´Aaishah na Hadiyth ya Abu Hurayrah:
”Tukafanya baadaye mto mmoja au mito miwili.”
na:
”Amrisha pazia ikatwe na kufanywe mito miwili inayokanyagwa chini.”
Katika hayo kuna dalili ya kujuzu kubaki kwa picha zilizotengenezwa ikiwa zimefanywa kuwa vitu vya chini kama tandiko au mto. Lakini hilo halifahamishi kuwa inajuzu kutengeneza picha katika vitu hivyo. Bali kutengeneza picha ni haramu kwa mtengenezaji wake katika hali yoyote ile. Akifanya hivyo, basi amefanya lililoharamishwa. Yule ambaye picha imefika kwake kisha akaifanya kuwa kitu cha kutandikwa chini, basi kwa kufanya hivyo ameondokewa na wajibu wa kukemea ovu juu yake.
Kiasi hiki kinatosha kwa mwenye uongofu – na Allaah ndiye Mwenye kutoa tawfiyq.
Muhusika: Imaam Muhammad bin ´Aliy ash-Shawkaaniy (afk. 1250)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Hukm-ut-Taswwiyr, uk. 35-38
Imechapishwa: 07/05/2026
https://firqatunnajia.com/08-picha-katika-vitu-vinavyotwezwa/