Miongoni mwa fadhilah za mwezi huu uliobarikiwa ni kwamba ndani yake thawabu huongezwa. Imepokelewa kwamba ´ibaadah za kujitolea hulipwa sawa na faradhi na faradhi hulipwa sawa na faradhi sabini.

Anayemfuturisha mfungaji hupata msamaha wa madhambi yake na kuachiliwa huru shingo yake kutokana na Moto. Aidha hupata mfano wa thawabu ya aliyefunga bila kupunguzwa chochote katika thawabu yake. Haya yote ni mema, baraka na manufaa yanayowashukia waislamu kwa kuingia kwa mwezi huu uliobarikiwa.

Kwa hiyo inapasa kwa muislamu kuupokea mwezi huu kwa furaha, bashasha na shangwe. Vilevile amshukuru Allaah kwa kuufikia na kumuomba msaada wa kuufunga na kutanguliza matendo mema ndani yake. Hakika ni mwezi mkubwa, msimu mtukufu na mgeni aliyebarikiwa kwa ummah wa Kiislamu. Tunamuomba Allaah atujalie sehemu ya baraka zake na manufaa yake. Hakika Yeye ni Msikivu, Mwenye kujibu. Himdi zote njema anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 16
  • Imechapishwa: 28/01/2026