Miongoni mwa fadhilah za mwezi huu ni yale aliyoyabainisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth Swahiyh, kama ilivyokuja kwa al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameleeza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Inapokuja Ramadhaan basi hufunguliwa milango ya Pepo, hufungwa milango ya Moto na mashaytwaan hufungwa.”[1]
Hadiyth hii ikafahamisha fadhilah kubwa za mwezi huu uliobarikiwa:
1 – Kufunguliwa kwa milango ya Pepo ndani yake. Hilo ni kwa sababu ya wingi wa matendo mema yanayofanywa ndani yake na ambayo husababisha kuingia Peponi. Allaah (Ta´ala):
ادْخُلُوا الْجَنَّةَ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
”Ingieni Peponi kwa sababu ya yale mliyokuwa mkitenda!”[2]
2 – Kufungwa kwa milango ya Moto katika mwezi huu. Hilo ni kwa kwa sababu ya kupungua kwa maasi yanayosababisha kuuingiza. Allaah (Ta´ala):
فَأَمَّا مَن طَغَىٰ وَآثَرَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا فَإِنَّ الْجَحِيمَ هِيَ الْمَأْوَىٰ
”Yule aliyepindukia mipaka kuasi na akapendelea maisha ya dunia, basi hakika Moto ndio makazi yake.”[3]
وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَإِنَّ لَهُ نَارَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا
“Yeyote atakayemuasi Allaah na Mtume Wake, basi hakika atapata Moto wa Jahannam hali ya kudumu humo milele.”[4]
Ama aliyeasi na akatanguliza maisha ya dunia, basi hakika Jahannam ndiyo makazi.
3 – Kufungwa kwa mashaytwaan ndani yake, kwa maana hufungwa na kufungwa nguvu. Kwa maana nyingine hawawezi kuwahadaa waislamu na kuwashawishi kwa maasi wala kuwazuia na matendo mema, kama walivyokuwa wakifanya katika miezi mingine. Kuzuiwa kwao katika mwezi huu uliobarikiwa ni rehema kwa waislamu ili wapewe fursa ya kufanya mema na kufutiwa maovu.
[1] al-Bukhaariy (1898), (1899) na Muslim (1079).
[2] 16:32
[3] 79:37-39
[4] 72:23
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 16
- Imechapishwa: 28/01/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 16
Imechapishwa: 28/01/2026
https://firqatunnajia.com/07-mwezi-ambao-milango-ya-pepo-hufunguliwa-na-milango-ya-moto-ikafungwa/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket