Baadhi ya waliokuwa wanayajua haya wamepingana na Hadiyth:

“Mola Wetu (Tabaarak wa Ta´ala) huteremka katika mbingu ya chini pale kunapobaki theluthi ya mwisho ya usiku na husema: “Ni nani mwenye kuniomba nimuitikie? Ni nani mwenye kuniomba nimpe? Ni nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe?”[1]

na wakasema kuwa theluthi ya usiku inatofautiana kutoka mji mmoja kwenda mwingine – kwa hiyo haiyumkiniki kushuka kukawa wakati maalum.

Ni jambo linalotambulika kihakika ubaya wa upingaji kama huu. Isitoshe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na makhaliyfah wake waongofu iwapo wangelimsikia mmoja anayepinga namna hiyo, wasingemjadili peke yake bali pia kumuadhibu na kumzingatia mtu huyo ni miongoni mwa wanafiki na wenye kukadhibisha.

[1]al-Bukhaariy (7494) na Muslim (758).

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Fadhwl ´Ilm-is-Salaf ´alaa ´Ilm-il-Khalaf, uk. 48
  • Imechapishwa: 14/09/2021