Chengine chote chenye kuzidi hapo hakina haja na kinamshughulisha mtu na yale ambayo ni muhimu zaidi. Kuna khatari hata ubobeaji kama huu ukampelekea kutilia mashaka maharib za waislamu, kama ilivyowatokea wanazuoni wengi. Matokeo yake watu wakaanza kufikiria kuwa Maswahabah na Taabi´uun waliswali kuelekea upande wa makosa, madai ambayo ni batili. Ahmad amekemea kujengea hoja kwa alama ya unajimu na akasema:

“Kitu pekee kilichopokelewa ni kwamba Qiblah kiko baina ya Mashariki na Magharibi.”

Bi maana hakukupokelewa chochote juu ya kwamba mswaliji aswali kuelekea alama ya unajimu au alama nyingine ya nyota. Ibn Mas´uud alimkemea Ka´b kusema kwamba vituo vya mwezi vinazunguka. Maalik pia na wengine wamekaripia jambo hilo. Imaam Ahmad amewakemea wanajimu waliosema kwamba kupondoka kunatofautiana kutoka nchi hadi nyingine. Huenda ukaripiaji wao wa upekuzi kama huu ni kwa sababu Mitume hawakuzungumzia mambo kama haya, ingawa wanajimu wenyewe wanajiona ni wenye kupatia mia kwa mia katika jambo lao, sababu nyingine kujishughulisha na mazungumzo hayo pengine yakampelekea mtu katika uharibifu mkubwa.

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Fadhwl ´Ilm-is-Salaf ´alaa ´Ilm-il-Khalaf, uk. 47-48
  • Imechapishwa: 14/09/2021