Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Yeye ndiye alivunja picha za watu hawa wema.

MAELEZO

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivunja picha za masanamu siku ya kuteka Makkah. Alipoingia katika Ka´bah, kulikuwa pembezoni mwake na ndani yake masanamu 360. Akiyavunja (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) kwa bakora yake na huku akisoma maneno Yake (Ta´ala):

وَقُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ ۚ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا

“Na sema: “Haki imekuja na ubatilifu umetoweka. Hakika ubatilifu daima ni wenye kutoweka.” (17:81)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Utaymiyn
  • Mfasiri: Fitqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 20
  • Imechapishwa: 23/04/2022