4 – Kipengele cha nne: Kila sifa ya Allaah inaelekezewa maswali matatu:

1 – Ni ya kikweli na kwa nini?

2 – Inafaa kuifanyia namna na kwa nini?

3 – Inalinganishwa na sifa za viumbe na kwa nini?

Jawabu ya swali la kwanza ndio la kikweli. Msingi wa maneno ni ukweli. Mtu haachi ukweli huo isipokuwa kwa dalili sahihi inayozuia kutokamana na jambo hilo.

Jawabu ya swali la pili ni kwamba haijuzu kuzifanyia namna. Amesema (Ta´ala):

وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا

“… na wala hawawezi kumzunguka Yeye wote kiujuzi.”[1]

Isitoshe akili haiwezi kutambua namna zilivyo sifa za Allaah.

Jawabu ya swali la tatu ni kwamba hazifananishwi na sifa za viumbe. Amesema (Ta´ala):

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ

”Hakuna chochote kinachofanana Naye.”[2]

Jengine ni kwamba Allaah anastahiki ukamilifu ambao hauna mwisho juu yake. Hawezi kufananishwa na viumbe kwa sababu ni wapungufu.

Tofauti kati ya kuzifananisha sifa za Allaah (التمثيل) na kuzifanyia namna sifa za Allaah (التكييف) ni kwamba kufananisha ni kutaja namna ilivyo sifa ya Allaah hali ya kuiwekea sharti na chenye kufanana na sifa hiyo na kufanya namna na kutaja namna ilivyo sifa ya Allaah pasi na kuiwekea sharti na chenye kufanana na sifa hiyo.

Mfano wa kulinganisha ni mtu kusema kuwa mkono wa Allaah ni kama mkono wa mtu. Mfano wa namna ni mtu kufikiria kuwa mkono wa Allaah una namna fulani usiyolingana na mikono ya viumbe. Haijuzu kufikiria namna hii.

[1] 20:110

[2] 42:11

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 26-27
  • Imechapishwa: 09/10/2022