Hukumu ya kukaa vijiweni kwa mujibu wa mfunzo ya Uislamu

Swali: Wako wanaosema kuwa inachukiza kukaa vijiweni hata kama watu wataipa njia haki yake na bora ni kuacha kufanya hivo.

Jibu: Udhahiri wa Hadiyth unaonyesha kuwa muumini anatakiwa kujiepusha na vijiwe. Kwa sababu pengine asiipe barabara haki yake. Kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Jiepusheni na kukaa.”

Lakini ikiwa wamelazimika au kwa msemo mwingine wanataka kukaa kijiweni na wanahitaji kufanya hivo, basi ni lazima waipe njia haki yake. Kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vinginevyo kujiepusha ni bora kwao.

Swali: Maoni yanayosema kuacha kufanya hivo licha ya kuwa watu wataipa haki yake?

Jibu: Ni kheri na bora kwao. Kwa sababu pengine wasiipe njia haki yake na pengine wakadhoofika na wasiipe haki yake. Wakiwa na uhakika kuwa wataipa barabara haki yake basi ni jambo zuri. Lakini ni nani ana uhakika na nguvu ya jambo hilo?

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21977/حكم-الجلوس-في-الطريق-مع-اعطاىه-حقه
  • Imechapishwa: 09/10/2022