3 – Kipengele cha tatu: Sifa zilizothibitishwa (Thubuutiyyah) zimegawanyika sampuli mbili:

1 – Sifa za kidhati.

2 – SIfa za kimatendo.

Sifa za kidhati ni zile ambazo anasifika nazo milele. Kama vile usikivu na uoni.

Sifa za kimatendo zimefungamana na matakwa Yake; akitaka anazifanya na asipotaka hazifanyi. Kama vile kulingana juu ya ´Arshi na kuja.

Wakati mwingine sifa inaweza kuwa ya kidhati wakati huohuo kwa njia nyingine ikawa ya kimatendo. Ni kama maneno. Kwa kuzingatia msingi wa sifa ni ya kidhati. Kwa sababu Allaah alikuwa na bado ataendelea kuwa Mwenye kuzungumza. Na kwa kuzingatia kwamba anazungumza pale anapotaka ni sifa ya kimatendo. Kwa sababu maneno yamefungamana na utashi Wake ambapo anazungumza kwa yale anayotaka na pale anapotaka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 26
  • Imechapishwa: 09/10/2022