08. Kuwauliza familia ya maiti kama alikuwa anaswali

Swali 08: Je, inafaa kwa mwoshaji kuuliza familia ya maiti kama aliyekufa anaswali au haswali[1]?

Jibu: Midhali ni muislamu na wale waliomleta ni waislamu basi hakuna haja ya kuwauliza. Wako wanaochukulia wepesi jambo hilo na hivyo likapelekea katika fedheha. Vivyo hivyo wakati wa kumswalia. Hivyo haifai kuuliza juu yake ikiwa udhahiri wake ni Uislamu.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/106-107).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 15
  • Imechapishwa: 11/12/2021