Allaah ametuumba na akaturuzuku na hakutuacha bure tu. Ametuamrisha kumuabudu Yeye, kumtii na kutomuasi. Ametutumia Mtume ambaye ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amemteremshia Qur-aan ili tuongozwe nayo, kutendea kazi maamrisho yake na kujiepusha na makatazo. Yote hayo yanapitika kwa Mtume wa Allaah na Nabii na Mtume wa mwisho Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amekuja kuwafunza watu dini yao. Yeye ndiye Nabii wa mwisho, kiongozi wao na mbora wao.

Atayemtii Mtume huyu na kushikamana barabara na dini yake ataingia Peponi. Atayemuasi Mtume huyu na akapinda kutokamana na dini yake ataingia Motoni. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّا أَرْسَلْنَا إِلَيْكُمْ رَسُولًا شَاهِدًا عَلَيْكُمْ

“Hakika Sisi Tumekutumieni Mtume awe ni shahidi juu yenu… “

Bi maana kwa matendo yenu anashuhudia:

كَمَا أَرْسَلْنَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ رَسُولًا

“… kama Tulivyotuma kwa Fir’awn Mtume.”

Yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Mtume.

فَعَصَىٰ فِرْعَوْنُ الرَّسُولَ فَأَخَذْنَاهُ أَخْذًا وَبِيلًا

“Lakini Fir’awn alimuasi huyo Mtume, Tukamuadhibu adhabu kali sana.” (73:15-16)

Fir´awn akachukuliwa mchukuo wa kuangamizwa duniani kwa kuzamishwa na Aakhirah Moto unamsubiri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 15
  • Imechapishwa: 15/10/2016