Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Muislamu ni yule mwenye kuwasalimisha waislamu kwa ulimi na mkono wake na muhajiri ni yule mwenye kuyahama yale Allaah aliyokataza.”[1]

Bahz bin Hakiym amepokea kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake ambaye ameeleza kuwa alimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya Uislamu ambapo akajibu:

“Ni kuusalimisha moyo wako kwa Allaah (Ta´ala), kuuelekeza uso wako kwa Allaah (Ta´ala), kuswali swalah za faradhi na kutoa zakaah iliyofaradhishwa.”[2]

Ameipokea Ahmad.

Abu Qilaabah amepokea kutoka kwa mtu miongoni mwa watu wa Shaam ambaye amepokea kutoka kwa baba yake ambaye alimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu Uislamu ambapo akajibu:

“Ni kuusalimisha moyo wako kwa Allaah (Ta´ala) na waislamu wasalimike na ulimi na mkono wako.” Akasema: “Ni Uislamu upi bora?” Akajibu: “Imani.” Akauliza: “Ni nini imani?” Akajibu: “Ni kumwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Wake na kufufuliwa baada ya kufa.”[3]

MAELEZO

Mambo haya yanajulisha ule ueneaji na kwamba Uislamu umekusanya nguzo na mambo ambayo si nguzo. Muislamu wa kweli ni yule mwenye kutekeleza nguzo, anatekeleza yale ambayo Allaah amemuwajibishia, anajizuia mikono yake kutokamana na dhuluma na kuishambulia mipaka ya Allaah.

[1] al-Bukhaariy (6484) na Muslim (41).

[2] Ahmad (3/5), Ibn Hibbaan (1/376) na al-Haakim (4/643).

[3] Ahmad (4/114)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fadhwl-il-Islaam, uk. 13
  • Imechapishwa: 25/10/2020