Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Allaah (Ta´ala) amesema:

فَإِنْ حَاجُّوكَ فَقُلْ أَسْلَمْتُ وَجْهِيَ لِلَّـهِ وَمَنِ اتَّبَعَنِ

“Na wakikuhoji, basi sema: “Nimejisalimisha kwa Allaah kikamilifu na wale walionifuata.” (03:20)

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Uislamu ni kushuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, kusimamisha swalah, kutoa zakaah, kufunga Ramadhaan na kuhiji kwenye Nyumba ukiweza kuiendea.”[1]

MAELEZO

Hili ndio jibu la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akimjibu Jibriyl (´alayhis-Salaam) wakati alipomuuliza kuhusu Uislamu ambapo akajibu kwa jawabu hili, kama ilivyokuja katika Hadiyth ya Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na ndani yake imekuja:

“Uislamu ni kushuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, kusimamisha swalah, kutoa zakaah, kufunga Ramadhaan na kuhiji kwenye Nyumba ukiweza kuiendea.”

Hii ndio maana ya Uislamu kwa nguzo zake. Uislamu umeenea na umekusanya kila ambacho amekiamrisha Allaah na Mtume wake na kujiepusha na kila alichokataza Allaah na Mtume wake. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ

 “Hakika dini mbele ya Allaah ni Uislamu.” (03:19)

Lakini hizi ni nguzo zake. Kitu kinaweza kufasiriwa kwa nguzo zake kama ambavo kinaweza pia kufasiriwa kwa sehemu zake zote.

[1] al-Bukhaariy (4777) na Muslim (102).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fadhwl-il-Islaam, uk. 11
  • Imechapishwa: 12/10/2020