04. Zama zinavyokwenda ndivo hali itazidi kuwa mbaya

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Muhammad bin Wadhdhwaah ameeleza jinsi Hudhayfah alivyokuwa akiingia msikitini na akiyasema haya. Akasema:

“Sufyaan bin ´Uyaynah ametueleza, kutoka kwa Mujaalid bin Sa´iyd, kutoka kwa ´Aamir ash-Sha´biy, kutoka kwa Masruuq ambaye ameeleza kuwa ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Hakuna mwaka unaokuja isipokuwa ulio baada yake ni mbaya zaidi. Simaanishi kuwa kuna mwaka wenye kunyesha zaidi kuliko mwingine au wenye rotuba zaidi kuliko mwingine wala kiongozi ambaye ni bora kuliko mwingine. Ninachomaanisha ni kuondoka kwa wanazuoni wenu na wabora wenu. Kisha kutajitokeza watu ambao watayakisia mambo kwa matamanio yao ambapo watauharibu Uislamu na uangamie.”[1]

[1] al-Bid´ah, uk. 61-62.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fadhwl-il-Islaam, uk. 10
  • Imechapishwa: 12/10/2020