Swali: Kuhusiana na kasi kubwa, umetaja kwamba kikomo cha kasi kinapaswa kufatwa, kama mfano wa 120 km/h. Jengine ni kwamba gari zinatofautiana. Gari nzuri inakuwa kana kwamba imesimama wakati inaenda mpaka kwenye 120 km/h na haizingatiwi kuwa ni kasi kubwa. Je, katika hali hiyo ni kosa mtu akaendesha mpaka 140 km/h au 150 km/h?

Jibu: Kasi inaamuliwa na mahakama. Kimsingi ni kwamba ni lazima kwa mtu kuifata, kwa sababu ni jambo linalotokamana na mtawala. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ

”Enyi mlioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.”[1]

Lililo la lazima kwetu sisi raia ni kutekeleza yale yaliyoamrishwa na watawala. Hata kama gari ni imara na mtu hahisi kwenda kwake kasi, kinachozingatiwa ni ile kasi. Hata gari hii ambayo iko imara ni khatari endapo tairi litapata pancha. Hata kama tairi liko salama hakuna awezaye kudhamini juu ya usalama wa dereva endapo ngamia au mnyama mwengine atajitokeza mbele yake.

Muulizaji: Nakusudia barabara kuu ambazo zimezungushiwa fensi za vyuma.

Ibn ´Uthaymiyn: Kwa hali yoyote ni kwamba msingi ni kwamba mtu anapaswa kufata taratibu za nchi. Huu ndio msingi.

[1] 04:59

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (8 A)
  • Imechapishwa: 12/10/2020