Ruqayyah bint Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

Mama yake alikuwa ni Khadiyjah.

Ibn Sa´d amesema:

”Aliolewa na ´Utbah bin Abiy Lahab kabla ya unabii.”

Usahihi ni kwamba ilikuwa ni kabla ya Hijrah. Wakati kulipoteremka Aayah:

تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ

”Imeangamia mikono miwili ya Abu Lahab na ameangamia.”[1]

ndipo Abu Lahab akasema:

”Sitaki chochote kuhusiana na wewe mpaka kwanza umtaliki msichana wake.”

Hivyo akamwacha kabla ya kumwingilia.

Akaingia katika Uislamu pamoja na mama yake na dada zake wengine. Kisha akaolewa na ´Uthmaan[2].

Ibn Sa´d amesema:

”Alihajiri pamoja naye Hijrah zote mbili kwenda Uhabeshi.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Ndio wa mwanzo kuhajiri kwa ajili ya Allaah baada ya Luutw.”

Alimzaa ´Abdullaah kutoka kwa ´Uthmaan na alikuwa akitumia kunyah yake. Alipokuwa na miaka sita, jogoo akomdonoa usoni. Uso wake ukawa na shimo na hivyo akafa.

Kisha akahajiri kwenda al-Madiynah baada ya ´Uthmaan.

Akagonjweka kabla ya vita vya Badr. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwacha ´Uthmaan amshughulikie. Akafariki wakati ambapo waislamu walipokuwa wanapigana vita vya Badr.

[1] 111:01

[2] at-Twabaqaat al-Kubraa (8/36).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (2/250-252)
  • Imechapishwa: 12/10/2020