07- Siku moja (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali juu ya minbari (na katika upokezi mwingine ya kwamba ilikuwa na ngazi tatu[1]). Alisimama juu yake akaleta Takbiyr na watu nyuma yake wakaleta Takbiyr. Wakati amesimama juu yake akarukuu. Kisha akainuka. Halafu akainuka na kushuka kinyumenyume mpaka akasujudu kwenye kitako cha minbari. Kisha akarudi na akafanya katika Rak´ah ya pili kama alivyofanya katika Rak´ah ya kwanza mpaka alipomaliza kuswali. Halafu akawageukia watu na kuwaambia:

“Enyi watu! Nimefanya hivi ili mnifuate na mjifunze swalah yangu.[2]

[1] Hii ndio Sunnah minbari iwe na ngazi tatu na si zaidi ya hapo. Minbari kuwa na zaidi ya ngazi tatu ni Bid´ah iliyoanzishwa na Banuu Umayyah. Minbari kama hii mara nyingi huzikata safu. Ili kuliepuka tatizo hilo inawekwa upande wa magharibi wa msikiti au wa Mihrab. Hii ni Bid´ah nyingine nayo. Bid´ah nyingine ni kule kuitengeneza kama balkoni ikawa imepandishwa kwenye ukuta wa kusini. Njia ya kupanda kuiendea ni kupitia ngazi zilizoko ukutani. Na uongofu bora ni wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tazama “Fath-ul-Baariy” (02/331)

[2] al-Bukhaariy, Muslim (ambaye amepokea huo upokezi mwingine) na Ibn Sa´d (1/253). Imetajwa katika ”al-Irwaa’” (545).

 

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 71-72
  • Imechapishwa: 13/10/2016