Qur-aan tukufu ndio tukufu zaidi katika vitabu hivi vinne, bora, ya mwisho, inayovifuta, inayovihukumu, kuvitawala na kuvisadikisha. Amesema (Ta´ala):

وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ

“Tumekuteremshia Ukumbusho ili uwabainishie watu yale yaliyoteremshwa kwao.”[1]

Kwa hivyo ni lazima kuiamini Qur-aan hii tukufu kwa njia maalum kwa kuitakidi ya kwamba ndio kitabu bora, chenye kheri zaidi, cha mwisho, inayovifuta, kusadikisha maelezo yake, kutekeleza hukumu zake, kutendea kazi zile Aayah zake zilizo wazi, kuamini zile Aayah zisizokuwa wazi, kusimama kwenye mipaka yake, kuwaidhika na mawaidha yake, kuzingatia maana yake, kuhukumiwa nayo pamoja na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati wa kutofautiana. Amesema (Ta´ala):

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا

”Mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamuamini Allaah na siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri kabisa.”[2]

[1] 16:44

[2] 04:59

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Iymaan – Haqiyqatuhu wa Nawaaqidhwuh, uk. 14
  • Imechapishwa: 21/03/2023