06. Msingi wa tatu ambao ni kuamini Vitabu vilivyoteremshwa

Ni kuamini kwa kukata na kusadikisha ya kwamba Allaah (Ta´ala) amewateremshia vitabu Manabii na Mitume Yake, kwamba ni haki, uongofu na nuru ambavyo vinahukumu kati ya watu katika yale wanayotofautiana. Amesema (Ta´ala):

كَانَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً فَبَعَثَ اللَّـهُ النَّبِيِّينَ مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَأَنزَلَ مَعَهُمُ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِيَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ فِيمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ

“Watu walikuwa ummah mmoja kisha Allaah akawatuma Mitume hali ya kuwa ni wabashiriaji na waonyaji na Akateremsha pamoja nao Kitabu kwa haki ili kihukumu kati ya watu katika ambayo wamekhitilafiana kwayo.”[1]

Kwa hiyo tunaamini vitabu hivi kwa njia ya ujumla na pia tunaamini vile vilivyotajwa ndani ya Qur-aan kwa upambanuzi. Navyo ni vitabu vinne vitukufu; at-Tawraat, Injiyl, az-Zabuur na Qur-aan. Vivyo hivyo sahifa za Ibraahiym na Muusa (Swalla Allaahu ´alayhimaa was-Salaam).

Vikubwa katika vitabu hivo vinne ni vitabu viwili; Tawraat na Qur-aan. Mara nyingi Allaah anavitaja kwa pamoja ndani ya Kitabu Chake kitukufu. Amesema (Ta´ala):

فَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا لَوْلَا أُوتِيَ مِثْلَ مَا أُوتِيَ مُوسَىٰ ۚ أَوَلَمْ يَكْفُرُوا بِمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ مِن قَبْلُ ۖ قَالُوا سِحْرَانِ تَظَاهَرَا وَقَالُوا إِنَّا بِكُلٍّ كَافِرُونَ

”Basi ilipowajia haki kutoka Kwetu, walisema: “Kwa nini hakupewa mfano wa yale aliyopewa Muusa?” Je, kwani hawakuyakufuru yale aliyopewa Muusa kabla? Wakasema: ”Sihri mbili zimesaidiana na wakasema: “Hakika sisi kwa vyote viwili ni wenye kuvikanusha.”[2]

ثُمَّ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ تَمَامًا عَلَى الَّذِي أَحْسَنَ وَتَفْصِيلًا لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً لَّعَلَّهُم بِلِقَاءِ رَبِّهِمْ يُؤْمِنُونَ وَهَـٰذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ فَاتَّبِعُوهُ وَاتَّقُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ

“Kisha Tulimpa Muusa Kitabu kutimiza [neema] juu ya yule aliyefanya vitendo vyema na chenye kupambanua wazi kila kitu na kiwe ni mwongozo na rehema ili wapate kuamini kukutana na Mola wao. Na hiki ni Kitabu tumekiteremsha kilichobarikiwa, basi kifuateni na mumche Allaah mpate kurehemewa.”[3]

[1] 02:213

[2] 28:48

[3] 06:154-155

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Iymaan – Haqiyqatuhu wa Nawaaqidhwuh, uk. 13
  • Imechapishwa: 21/03/2023