07. Ni ipi hukumu ya kamari na yule anayedai kuwa inafaa?

Swali 07: Ni ipi hukumu ya kamari na yule anayedai kuwa inafaa?

Jibu: Kamari ni kitu kinatambulika kwa watu wengi na maana yake ni pale ambapo wanatofautiana watu wawili ambapo mmoja wao anasema: “Ikiwa mambo ni hivyo ulivosema, basi mimi nakupa hiki na hiki, na kama mambo ni vile ulivosema, basi nawe utanipa hiki na hiki.” Jambo hilo halijuzu kwa sababu ni kamari, jambo ambalo Allaah (´Azza wa Jall) ameliambatanisha na pombe. Amesema (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ

“Enyi walioamini! Hakika si vyenginevyo pombe na kamari na kuabudu masanamu na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli ni uchafu kutokana na kazi ya shaytwaan, hivyo basi jiepusheni navyo mpate kufaulu. Hakika si venginevyo shaytwaan anachotaka kukutilieni kati yenu uadui na bughudha katika pombe na kamari na akuzuieni kumdhukuru Allaah na swalah, basi, je, mtakoma?”[1]

Kutokana na hilo kamari hii ni haramu. Kitendo cha baadhi ya watu kuona kuwa inafaa, haizidishi kitu isipokuwa ubaya tu. Kwa sababu ameifanya batili kuwa ni haki na ameipa jina lisilokuwa lake. Amelipamba na kuifanya ndio suluhisho. Kwa hivyo anakuwa ni mwongo katika yale aliyoyadai na mwenye kuhadaa katika yale anayoyadhihirisha – tunamuomba Allaah usalama na afya.

[1] 05:90-91

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah Muhimmah, uk. 14-15
  • Imechapishwa: 26/02/2023