06. Ni ipi hukumu ya kukodisha maduka ya biashara kwa wale wanaouza sigara, nyimbo na kanda za video zisokuwa nzuri au benki za ribaa?

Swali 06: Ni ipi hukumu ya kukodisha maduka ya biashara kwa wale wanaouza sigara, nyimbo na kanda za video zisokuwa nzuri au benki za ribaa?

Jibu: Hukumu ya kukodisha maduka haya inabainika katika maneno Yake (Ta´ala):

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖوَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ

“Saidiane katika wema na kumcha Allaah na wala msisaidiane katika dhambi na uadui.”[1]

Kutokana na hili kukodisha maduka kwa ajili ya utumiwaji uliyotajwa katika swali ni haramu. Kwa sababu ni kusaidiana katika dhambi na uadui.

[1] 05:02

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah Muhimmah, uk. 14
  • Imechapishwa: 26/02/2023