2- Kupupia kuyafanyia kazi mafunzo ya Kiislamu
Upupuaji huu umekusanya kutendea kazi yale mambo yaliyowajibishwa na Shari´ah kama mfano vipindi vitano vya swalah, kuwatendea wema wazazi wawili na mengineyo. Vivyo hivyo kumekusanya kupupia kuzifanyia kazi Sunnah na kuzifufua kati ya watu kiasi na vile muislamu atakavyoweza. Mfano wa mambo hayo ni swalah za sunnah, Witr, kusimama usiku, swawm za sunnah na mengineyo. Mtu anatakiwa kupupia kuyatekeleza.
Abu ´Abdir-Rahmaan as-Sulamiy (Rahimahu Allaah) amesema:
“Wametuhadithia wale ambao walikuwa wanatufundisha Qur-aan – yaani Maswahabah – walikuwa wakisoma kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo wakijifunza Aayah kumi basi hawazivuki mpaka watendee kazi yale matendo yaliyomo ndani yake. Hivyo tukajifunza Qur-aan na matendo kwa wakati mmoja.”[1]
Huu ndio mfumo wa Salaf (Rahimahumu Allaah). Walikuwa wakiifuatishia elimu matendo. Kwa sababu kuifanyia kazi elimu kunamwepusha mtu na makemeo makali ya adhabu inayompelekea mtu kwa kule kuacha kwake kitendo cha lazima pale Allaah (Ta´ala) aliposema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ
“Enyi walioamini! Kwanini mnasema yale msiyoyafanya? Ni chukizo kubwa kabisa mbele ya Allaah kwamba mnasema yale msiyoyafanya.”[2]
Sababu nyingine ni kwamba mtu kuitendea kazi elimu kunamwepusha na sifa mbaya ambayo Allaah amewasifu kwayo mayahudi pale (´Azza wa Jall) aliposema:
مَثَلُ الَّذِينَ حُمِّلُوا التَّوْرَاةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا ۚ بِئْسَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ
“Mfano wa wale waliobebeshwa Tawraat kisha wasiibebe ni kama mfano wa punda anayebeba vitabu vikubwavikubwa. Ubaya ulioje mfano wa watu waliokadhibisha Aayah za Allaah; na Allaah haongoi watu madhalimu.”[3]
Isitoshe kutendea kazi elimu kunamfanya mtu kufika katika yale malengo aliyokuwa anataka kufika kwa ajili ya kujifunza elimu. al-Fudhwayl bin ´Iyaadhw (Rahimahu Allaah) amesema:
“Hatoacha mwanachuoni kuwa mjinga kwa yale aliyojifunza akayajua mpaka ayatendee kazi. Atakuwa mwanachuoni pale atapoyafanyia kazi.”[4]
Da´wah ya Salafiyyah inatilia umuhimu na kuchunga msingi huu. Vilevile inawahimiza watu kujishughulisha nao. Hakika mtu kujishughulisha na matendo kuna manufaa zaidi kuliko kujishughulisha na mambo yasiyokuwa na faida katika maneno yanayofaa na mambo mengineyo.
[1] Ibn Jariyr katika ”Tafsiyr” yake (01/80).
[2] 61:02-03
[3] 62:05
[4] Ameyatoa al-Khatwiyb al-Baghdaadiy katika ”Iqtidhwaa´-ul-´Ilm al-´Amal”, uk. 37.
- Muhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 32-34
- Imechapishwa: 04/08/2020

Muhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 32-34
Imechapishwa: 04/08/2020
https://firqatunnajia.com/07-msingi-wa-pili-kupupia-kuyatendea-kazi-mafunzo-ya-uislamu/